Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI ENEO LA KWALA KIBAHA

 




SERIKALI imewataka wananchi kutumia fursa zilizopo kwenye eneo la uwekezaji la Kwala wilayani Kibaha Mkoani Pwani baada ya kuingia mikataba ya uwekezaji wa ardhi kwa wawekezaji mbalimbali kwenye  eneo lenye ukubwa wa hekari 2,500.


Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji wakati wa hafla ya kukabidhi kiwanja namba 1 kitalu B kwenye eneo hilo la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa mwekezaji wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda.


Aidha alisema kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimevunja rekodi kwa kusajili miradi 266 katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni usajili wa miradi mingi ya uwekezaji kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja.


Kijaji alisema kuwa uwingi wa miradi hiyo haijawahi kusajiliwa kwa muda mfupi ndani ya mwaka mmoja tangu nchi imepata uhuru ambapo utawala wa Rais umefanya ndani ya mwaka mmoja ambapo mradi huo wa wawekezaji toka nchi ya China na ni ushuhuda wa mkakati wa Taifa wa ajenda ya viwanda kufikia pato la kati ifikapo mwaka 2025.


"Manufaa ya uwekezaji huu ni uhakika wa soko la malighafi ambapo mikataba iloyosainiwa ni ya viwanda vya kuchakata mazao ambapo Watanzania wanakwenda kunufaika na soko kwani kwa sasa liko hapa tuanze nyumbani tutambue umuhimu wa mradi hata kujifunza kichina madiwani wawape elimu wakinamama na watoto juu ya umuhimu wa kutumia eneo hilo la uwekezaji la Kwala,"alisema Kijaji. 


Naye katibu mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Profesa Tobias Kaiyarara   alisema kuwa upatikanaji wa ardhi ni jambo kubwa kuliko kitu chochote ndiyo maana sheria zinabadilishwa ili ardhi ipatikane haraka ili mradi ufanyike kwa haraka.


Kwa upande wake Mwakilishi wa wa Sino Tan Kibaha Jensen Huang alisema kuwa mradi huo umegharimu dola za Marekani 150 ikiwa ni gharama za upatikanaji ardhi, miundombinu na vifaa na utatoa ajira 100,000 za moja kwa moja.


Kunenge alisema mkoa una viwanda 1,453 na 87 viwanda vikubwa na kwa kutumia mikakati kuvutia wawekezaji wawekeze viwanda vikubwa na vya kati viwe vikubwa na Rais aliahidi kipaumbele kwa kutoa nishati ya umeme, gesi na miundombinu barabara na maji nishati ikiwa na maji na barabara watavutiaji wawekezaji watakuwa wengi kwani miundombinu ina mchango mkubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI