Header Ads Widget

WANANCHI WAMWANGUKIA MHE. RIDHIWANI KURUDISHA ARDHI ILIYOKALIWA NA MWEKEZAJI BILA KUENDELEZA

 



Na Bwanku M Bwanku.


Jana Ijumaa Machi 04, 2022 Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete aliendelea na ziara yake katika kata ya Vigwaza ambapo alitembelea shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kufanya mikutano mitatu mikubwa katika Vijiji vya Buyuni, Kwazoka na Vigwaza Kambini ambapo alitumia mikutano yote hiyo kuwapa nafasi Wananchi kueleza kero zao halafu Yeye na timu aliyoambatana nayo ya Wataalamu wa Halmashauri ya Chalinze kutolea ufafanuzi wa kero zote pamoja na kuwaeleza Wananchi mipango yote mikubwa inayopangwa na Serikali yao ya Rais Samia kwenye sekta zote za Kijamii na uchumi.



Akiwa Kijiji cha Kwazoka, Mhe Ridhiwani Kikwete alipewa kero kubwa iliyoelezwa kwa uchungu mkubwa na Wananchi hao kwa kuiomba Serikali kurejesha eneo la Hekta 280 ambalo limeshindwa kuendelezwa na Mwekezaji wa Machine Consultant Ltd (BARUTI) ambao walipewa eneo hilo toka mwaka 1992 kwa ajili ya kufanyia uwekezaji lakini miaka 30 mpaka sasa hawajaweza kufanya uwekezaji wowote hivyo Wananchi kuiomba Serikali kuangalia namna ya kurudisha eneo hilo ili Wananchi walitumie kwa maendeleo maana Wawekezaji hao wameonyesha waziwazi kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu sana.


Kero hiyo ilijibiwa vyema ya Mhe. Ridhiwani kwa kuagiza Wataalamu wa Ardhi wa Chalinze kuona namna ya kuishauri Wizara yake ili eneo hilo lifutwe na kurudishwa kwa Wananchi kwa matumizi ya maendeleo maana kwasasa limekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa.



Kuhusu kero kubwa pia ya mgogoro mkubwa wa Ardhi aliyolalamikiwa na Wananchi eneo la Kiloweko na kati ya Kwazoka na Chaulu, Mhe Ridhiwani akayachukua hayo yote kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi Wananchi kurudisha majibu haraka iwezekanavyo.


Migogoro mingine mikubwa ya ardhi aliyoelezwa Mhe. Ridhiwani akiwa katika mkutano wa 3 katika Kijiji cha Vigwaza Kambini ni pamoja na ule wa kati ya Kijiji cha Vigwaza na Visenzi na Vigwaza na Mnindi ambapo alitoa maelekezo kwa Wataalamu wake wa Wizara kufika maeneo hayo kumaliza migogoro hiyo.



Mhe. Ridhiwani alitumia mikutano hiyo yote kuwaeleza Wananchi kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Rais Samia kupeleka fedha katika Wilaya ya Chalinze kutekeleza miradi mikubwa ya elimu, miundombinu, afya, umeme, upimaji na urasimishaji ardhi, kusaidia vikundi vya Wajasiriamali wadogo kupata mikopo na mambo mengine.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI