Header Ads Widget

WANANCHI MKOANI KAGERA WASHAURIWA KUJENGA UTAMADUNI WAKUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA.

 



Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.


Wananchi mkoani Kagera wameshauriwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao  kila mara  kwani itawasaidia kujua hali ya miili yao na afya zao kwa ujumla.


Kauli hiyo imetolewa na afisa biashara mkoa wa Kagera Issaya Tendega  akimwakilisha katibu tawala wa mkoa wa Kagera Prf.Faustine Kamuzola katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani  yenye kaulimbiu isemayo okoa maisha wekeza katika kutokomeza kifua kikuu nchini ambapo kwa mkoa wa kagera maadhimisho hayo imefanyika katika uwanja wa Mayunga ulipo Manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali , taasisi binafsi,wadau wa afya  pamoja wananchi. 


“Nachukua nafasi hii kuwasihi wanchi wa mkoa wa Kagera kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kujua hali ya miili yao, ukipima afya ukakuta unamaambukizi unapata matibabu pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na ukikuta hauna maambukizi unaendelea kujikinga zaidi, upimaji wa magojwa haya ni bure kabisa hivyo tusisite kupima”.




Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa repoti ya shirika la afya dunia inasema kuwa watu zaidi ya 4000 upoteza maisha kila siku  duniani hivyo amewaomba wadau mbalimbali ambao wanania ya kuungana na serikali katika kupambana na ugojwa wa kifua kikuu na magonjwa mengine  kujitokeza ili kunusulu maisha ya wananchi.


Naye meneja wa  mradi wa  kifua kikuu, TB na HIV mkoani Kagera kwa upande wa The management and Development for Health (MDH) Kagera  Dr. Frenk  Malugu amewashukuru viongozi wa serikali mkoa wa kagera pamoja na watoa huduma ngazi ya jamii kwa kushirikiano wao katika  kuendeleza mapambano juu ya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaomba kuendelea kushirikiana ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.




“ Tumeweza kugundua wateja wengi wa kifua kikuu na kuvuka makadilio yetu na hii ni kutokana na msukumo wa watu kujitokeza kwa wingi kupima ugonjwa huu, mfano makadilio yetu hapo mwanzoni yalikuwa ni kugundua wateja kuanzia  820 kwa kila robo mwaka lakini  tumeweza kuibua wateja 1000 kwa upande wa mkoa wetu wa Kagera, tumeweza kufanya kazi hii kupitia misaada tunayotoa kwenye vituo vya afya tukisaidiana na serikali na kupitia watoa huduma wetu kwa ngazi ya jamii  ambao wanapatikana katiaka maeneo mnbali mbali ya mkoa huu” 


Kila ifiikapo tarehe 24 ya kila mwaka nchi mbalimbali ulimwenguni  uadhimisha siku ya kifua kikuu, kwa upande wa Tanzania maadhimisho hayo kitaifa yamegnyika mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa waziri wa afya Ummy Mwalimu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI