Kiwale ametoa Rai hiyo jana wakati wa mwendelezo wa Mafunzo ya Siku 10 ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na Halmashauri ya Mufindi Kwa kushirikiana na mradi wa YAM pamoja na taasisi ya Foex Community and wildlife conservation (FCWC).
Amewataka vijana waache kukaa Vijiweni na badala yake kutumia vizuri muda Kwa kufanya kazi za Kilimo na nyingine za ujasiriamali ambazo wakizingatia zitawatoa Katika dimbwi la umasikini wa kipato
Awali akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoanza Kiwale ambae ni mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji kwenye Kijiji Cha Igoda amesema mwanzo wananchi hawakumuelewa na walikuwa wakimuona kama amepitwa na wakati ila Sasa Kila mmoja anamuonea wivu Kwa pesa nzuri anayopata kwenye Kilimo cha Parachichi
Alisema kupitia zao hilo la Parachini hivi Sasa anakipato Cha uhakika kutoka na mti mmoja wa Parachichi unamwezesha kupata fedha zaidi ya shilingi 400,000 Kwa mchumo mmoja na yeye ana zaidi ya miti 2000 ya Parachichi hivyo Kwa mwaka anamiliki kipato Cha uhakika .
Alisema Kuhusu Soko la Parachichi ni zuri kwani Soko dogo la Parachichi Kwa ajili ya Kusafirisha kwenda nje ya Nchi lipo mkoani Njombe na kuwa Kwa mkulima Mwenye uwezo anaweza Kusafirisha mwenyewe kwenda kuuza nje .
Hata hivyo akishukuru Kwa elimu hiyo mshiriki Fex Kitinusa amesema elimu hiyo ni mtaji kwao na watakwenda kuitumia
Halmashauri ya Mufindi chini ya taasisi ya FCWC ndio watekelezaji wa mradi huo Youth Agency Mufindi kupitia ufadhili wa Finland ni mradi wa miaka minne utakaowafikia vijana 770 pamoja na watoto kwenye vijiji 16 vya kata za Luhunga , Mdabulo na Ihanu .
0 Comments