Header Ads Widget

AJALI YAUA 6..

 


WATU sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa Katika ajali iliyotokea Leo asubuhi Machi 29 baada ya gari aina ya fuso lenye namba za usajili T239 AFD kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye barabara kuu ya Soni -Mombo wilaya ya Lushoto mkoa wa Tanga .


 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga Safia Jongo amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo na kuwataka watumiaji wa barabara hasa wenye vyombo vya moto kuwa makini  pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani.


Kamanda Jongo amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa Katika Hospitali ya wilaya ya Lushoto na Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI