Header Ads Widget

UMMY MWALIMU AKABIDHI VIFAA TIBA ZAIDI YA 200 NA BIMA ZA AFYA 100 KWA WATU WENYE ULEMAVU

 



Teddy Kilanga _ArusHA



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema sekta ya afya wataendelea kuboresha huduma za utengamao nchini ili kuwa na takwimu sahihi za mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kuwawezesha waweze kumudu maisha kwa kutumia viungo alivyonavyo.



Akizungumza katika hafla ya kukabidhi miguu bandia ,viti mwendo,bima ya afya na fimbo za kutembele watu wenye ulemavu wasioona,Mwalimu alisema huduma za utengamao zinajumuisha huduma tiba za mazoezi ya viungo,kuzungumza na tiba kwa vitendo.



"Huduma hizo ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba visaidizi na nyinginezo katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya hivyo nakiri kuboresha huduma za utengamao na ninahaidi watu wote wenye ulemavu nchini watahakikisha wanapata takwimu sahihi za mahitaji halisi ya huduma  za utengamao,"alisema Waziri.



Mwalimu alisema kuna viashiria vinavyoonyesha uhitaji mkubwa  wa huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu ambapo watu hao wenye uhitaji hutoka kwenye makundi tofauti tofauti wakiwemo watu wenye magonjwa mbalimbali, watu wenye ulemavu na umri mkubwa pamoja na waliozaliwa na ulemavu.



Waziri alisema kutokana na sensa mwaka 2012 inaonyesha watu wenye ulemavu inaonyesha asilimia ya 5.8 ya Watanzania walikuwa na tatizo la ulemavu ambao wanaweza kuwa na mahitaji ya huduma hizo za vifaa tiba kwa hiyo walionyesha asilimia ya wazee ni 3.8 ambao pia wanahitaji huduma hizo za utangamao.





Aidha amekipongeza kituo cha Sanaa Tanzania  kwa kuwapa walemavu   ajira ya kutengeneza thamani za ndani na vitu mbalimbali ikiwemo urembo ambapo ajira hiyo inayowasaidia kupata kipato na kuweza  kujikimu kimaisha  



Waziri Ummy alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea kituo hicho ambapo alisema kuwa kinachofanyika ni jambo kubwa na zuri kwani angalau walemavu hawa wakiondoka hapo mwisho wa mwezi wana uhakika wa kupata mshahara unaoenda kuwasaidia angalau kupata mahitaji yao ya nyumbani.



“Mimi niwaombe mfanye kazi kwa bidii kwa bidii na kwa kujituma lakini pia msije mkasema kwamba ndio mmefika mwisho bali muwe na ndoto kubwa wengine mnaweza mkaja kumiliki maduka makubwa ya kutengeneza vifaa mbalimbali vya nyumbani,"alisema Ummy Mwalimu.



Alifafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mfuko wa watu wenye ulemavu ameshawaelekeza kila halmashauri kutenga asilimia mbili kupelekwa kwa watu wenye ulemavu hivyo viongozi mbalimbali wafanye wajibu wao kutekeleza agizo hilo lakini pia kufanya vizuri kama Sanaa Tanzania.






Kwa upande wake Meneja wa Sanaa Tanzania Sasuia Bruins alisema kuwa wanachukua watu ambao hakuna mtu anawataka na vitu ambavyo hakuna watu wanaovitaka na kutengeneza vitu ambavyo watu wanavinunua Duniani kote hivyo wanaoenda kufanya kazi na watu wenye ulemavu kwani wanauwezo mkubwa wakati mwingi kuliko watu wasio na ulemavu wa aina wowote.



“Wanaowezo mkubwa  hata zaidi ya watu wasio na ulemavu wowote labda ni kwasababu wana kiu ya kufanya kazi na kuwa huru bila kisaidiwa na mtu mwingine, mimi kwakweli toka nianze kufanya kazi na walemavu hawa nimeona wana uwezo mkubwa,”alisema Meneja huyo.



Aidha aliwasihi watanzania na jamii kwa ujumla kujaribu kuwakaribisha watu wenye ulemavu katika  makampuni yao kwani wataona na kufurahia wanachokifanya kwani wana akili na uwezo mkubwa wa kufanya kazi.





Naye Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo alisema amewashukuru wadau mbalimbali kujitokeza katika kuwasaidia baadhi ya vifaa tiba kwa watu wenye ulemavu wa wilaya ya Arusha kwani sio kitu rahisi.




Pia alisema alimshukuru Rais wa jamuhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani kuwa mstari wa mbele katika katika kuwahudumiwa wananachi na kusikiliza changamoto zao.



"Nitaendelea kushirikiana na serikali pamoja na viongozi mbalimbali kuhakikisha tunatatua changamoto za wananchi kwa lengo la kuleta maendeleo,"alisema Gambo Mbunge wa Arusha mjini.




Naye Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wilaya ya Arusha,Martha Mganga alisema anamshukuru mbunge huyo kwa kuwasaidia vifaa tiba mara tatu mfululizo limekuwa jambo la kihistoria kwao ambapo ni takribani jumla ya vifaa tiba hivyo ni 247 na bima za afya 100.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI