Adeladius Makwega-DODOMA
Katika sehemu ya kwanza ya matini juu ya Umahiri wa Machifu wa Kinyakyusa tuliona namna machifu hao walivyopambana na Wangoni na Wasangu na pia tuliona namna Waarabu walivyosuasua kuwavamia Wanyakyusa.
Leo tunaendelea kulitazama jambo hilo kufahamu je Waarabu waliwavamia Wanyakyusa? basi mwanakwetu ambatana nami neno kwa neno kutambua hilo.
Msito wa Waarabu kuwavamia Wanyakyusa katika eneo lao ulidumu mioyoni mwao lakini haukuwa msito mwema bali waliwachukia mno kwani eneo la Wanyakyusa lilikuwa na sifa zote za maeneo mengine ambayo Waarabu walifika. Mwaka 1884 kumbuka kile Kikao cha Berlini kwa hiyo Wamisionari walianza kukata mbuga za bara la Afrika kwa hiyo ndani ya Ngome ya Wanyakyusa Wamsionari walifika.
Kati ya mwaka 1887-1889 kulikuwa na mtafaruku baina ya Waarabu na Wazungu katika eno linalofahamika kama Karonga. Katika mgogoro huo baina ya Waarabu na jamaa wa Ulaya Mnyakyusa alikuwa upande wa Wazungu. Wazungu walipoleta askari katika maeneo hayo Wanyakyusa waliwapa hifadhi katika eneo ambalo sasa linafahamika kama Songwe na kulipokuwa na mgogoro Kusini basi Wanyakyusa waliwapa hifadhi Wazungu Kaskazini.
Katika kumbukumbu za Wanyakyusa inaaminika walifanyiwa uvamizi wa Henga ambapo walifanyiwa na Wangoni. Askari wa Wanyakyusa walifika kuokoa jahazi la uvamizi huo.
“Kuna mtafiti mmoja anayefahamika kama Monica Wilson alidai kuwa mahusiano ya Wanyakyusa na watu wa mbali hayakuwepo wakati jambo hilo kwa vigezo nilivyoeleza halina ukweli mtupu.”
Hayo yanasemwa na Mtafiti J Mwakipesile -UTANI RELATIONSHIP: NYAKYUSA 1972.
Katika hoja ya utani kwa kabila hili ni mkubwa mno, mathalani bibi akizungumza na mjukuu wkae wak iume anaweza kusema :
“Ndume gwangu”
Akimaanisha Mume wangu.
“Nkasi gwangu.”
Hapo Mjukuu akimwambia bibi yake kuwa mke wangu.
“Mwinagu”
Au
“Mkasi Mwinagu”
Hapo akimaanisha kuwa mjukuu wa kike anamwambia bibi yake kuwa yeye ni mke mwenzake.
“Nkasi gwangu”
Hapa babu anaweza kumuita mjukuu wake wa kike kuwa mke wangu.
Wanyakyusa wana utani kidogo baina ya mama na mtoto wake wa kiume akiwa na umri wa kati ya mwaka 1-6 anaweza kukishika kindunduli(sehemu ya siri ya mtoto w a kiume) chake na kukinusa na kusema ahaaa unanuka ebu nenda kaoge au anasema ebu twende ukaoge.
Jambo hilo linafanywa na mama anapomfundisha kijana wake wa kiume umuhimu wa usafi na jambo hilo mzazi wa kike ulifanya akiwa mwenyewe na mtoto wake wa kiume lakini ni mwiko kabisa mama huyu kufanya jambo kama hilo kwa binti yake wa kike.
Kwani huwa Wanyakyusa wanazo mbinu zingine za maelekezo ya usafi kwa mtoto wa kike. Hilo linafanyika kwa mtoto wa kiume baada ya muda mchache atakuwa mbali na mama yake kwa hiyo muda huo huwa wakati maalumu wa mama kumfundisha usafi kijana wake.
Basi mwanakwetu kwa leo naishia hapo.
Kipi kitaendelea subiri matini ijayo.
Nakutakia siku njema.
makwadeladaius@gmail.com
0717649257
0 Comments