Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akisalimiana na mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe leo ofisini kwake
.............,..........................
MWENYEKITI WA Taifa wa chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amekutana na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi na kukubaliana kufanya Siasa za kistarabu .mwandishi Francis Godwin Matukio Daima Media
Akizungumza leo Mara baada ya kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Katika Ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Iringa ,Mbowe alisema kama ambavyo alipata kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu baada ya kutoka gerezani anaona ni vema kuendelea kueneza ujumbe wa Siasa za kistarabu ili kukuza Demokrasia .
"Tulikuwa kwenye mkoa wenu wa Iringa na tumemaliza uwepo wetu Kwa Salama ndani ya mkoa huu tunashukuru na tumeona ni vizuri kukutana na Viongozi wa Serikali ya mkoa huu "alisema
Alisema kuwa mambo ambayo alizungumza na Rais Samia Ikulu juu ya kukijenga Tanzania na mambo ambayo yanapaswa kuzungumza Kila wakati na Kila mmoja wetu kuona Siasa zonazofanyika zinakuwa za kistarabu na zenye upendo na mshikamano badala ya kufanya Siasa za ugomvi .
Hata hivyo Mbowe alimshukuru mkuu wa mkoa wa Iringa Kwa kukubali kumkaribisha ofisini kwake na kufanya nae mazungumzo hayo .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alimpongeza Mbowe Kwa kufika ofisini kwake na kuwa Ofisi yake ni Ofisi ya umma inapokea Kila mmoja na kuwa busara zake za kufika ofisini ni wazi kiongozi huyo anahitaji Taifa kuwa na Siasa safi.
Alisema Mbowe amemuomba kuendelea kufanya Siasa safi ndani ya mkoa na yeye kama mkuu wa mkoa amemuhakikishia kufanya Siasa safi zenye tija Kwa ustawi wa Taifa .
Alisema kuwa Kwa mkoa wa Iringa utaendelea kudumisha Siasa safi zenye maendeleo kwani suala la Amani na utulivu ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mkoa na Taifa .
"Naamini Mbowe huu ndio mkoa wake wa kwanza kutembelea na kuja kukutana na mkuu wa mkoa niseme ni mwanzo mzuri na sisi kama mkoa tupo kuona Amani inadumishwa"
0 Comments