Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini , SACP. Wilbrod W. Mutafungwa, alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari ya kwamba Jeshi la polisi, Kikosi cha usalama Barabarani nchini lilianza Operesheni ya kukamata magari yote yanayowekwa ving'ora, vimulimuli na taa za kuongeza mwanga zinazofungwa kwenye magari knyume cha Sheria.
Kamanda aliueleza umma kuwa wamiliki na madereva wa magari, Bajaji na pikipiki hawaruhusiwi kuweka ving'ora, vimulimuli na taa za kuongeza mwanga na amewaataka wamiliki na madereva hao kuacha mara moja Uwekezaji wa vitu hivyo kwani wahalifu nap wanaweza kutumia mwanya huo kufanya uhalifu na kukimbia, na pia wanahalifu wanakuwa wanawahadaa askari barabarani kama Kamanda pia, ametoa takwimu ya opereshieni hii ambapo jumla ya ving'ora 1,527 vilitolewa kwenye magari, namba bandia 73 za magari ziling'olewa, ving'ora na vimulimuli 1,358 vilitolewa.
Kamanda alieleza kuwa operesheni hii ni endelevu na Jeshi la polisi litafanya Operesheni nchi nzima ili kutokomeza vitendo vya Uwekezaji wa namba za bandia, ving'ora na vimulimuli.
0 Comments