Morogoro
Mchakato wa kura za maoni za CCM umefanyika upya leo katika kata mbili za mkoa wa Morogoro baada ya kubainika kuwepo kwa hitilafu kwenye karatasi za kupigia kura hapo Jana.
Kata ya Mikese imehusika na kura za udiwani pekee, huku kata ya Tindiga ikihusisha kura za ubunge na udiwani, zote zikiwa ndani ya majimbo ya Morogoro kusini Mashariki na Mikumi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Nuru Ngereja amesema tayari majimbo 10 kati ya 11 yametoa matokeo huku Mikumi walichelewa kupata matokeo ya Jimbo kutokana na changamoto hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro
Baadhi ya waliotangazwa kuongoza ni Dkt. Abdulaziz Abood (Morogoro Mjini), Prof. Paramagamba Kabudi (Kilosa), Jonas Van Zeland (Mvomero), Hamis Taletale (Morogoro Kusini Mashariki),.
Salim Hasham Alaudin (Ulanga), Abubakary Asenga (Kilombero), Dkt. Rose Lwakatarare (Mlimba), Ahmed Shabiby (Gairo), Mecky Mdaku (Malinyi) na Zuberi Mfaume (Morogoro Kusini).
0 Comments