Header Ads Widget

DC JOKATE AHAMIA SEKTA YA UTALII TEMEKE.

 


Na:Shalua Mpanda-TMC


Sekta ya utalii imekuwa haizungumzwi sana ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Temeke ukilinganisha na maeneo mengine hapa nchini hali inayofanya baadhi ya wananchi kutotambua vivutio vinavyopatikana nndani ya Halmashauri ya manispaa hiyo.


Kwa kuliona hilo,Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo,jana Machi 10,2022 amefanya ziara ya kukagua maeneo ya fukwe zinazopatikana ndani ya manispaa ya Temeke.


Akiwa katika eneo la fukwe ya Kijiji cha wavuvi iliyopo Kurasini,Jokate amesema kuwa wanaangalia uwezekano wa kuboresha maeneo hayo ili yaweze kuleta tija na kuwa chanzo cha mapato kwa Serikali.




"Kuna nchi kama Singapore,Uturuki na nyinginezo zina maeneo kama haya na wanayatumia kwa ajili ya kutangaza utalii na kueleza historia yao,na sisi Temeke tuna historia yetu nzuri tu tunaweza kutembea na boti pembezoni mwa fukwe huku tukisimuliwa historia ya maeneo haya".Alisema Jokate


Kwa upande wake mtafiti huru wa kuendeleza makazi,fukwe na misitu Bw.Jafari Jongo amesema wakati wa kufanya utafiti katika kuendeleza utalii ndani ya miji,ameamua kuanza na wilaya ya Temeke kutokana na jiografia ya eneo lake kuwa na fursa ya kwenda pande zote pamoja na uwepo wa mito miwili ya Mzinga na Kizinga.



Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Wilaya kutoka Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) Bw.Francis Kiyondo ameeleza juu ya utunzaji na ufuatiliaji  wa maeneo hayo muhimu ambalo ni agizo la Serikali kupitia agizo la Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Baadhi ya maeneo yaliyotembelewa na Mkuu huyo katika ziara hiyo ni Kijiji cha Wavuvi Kurasini pamoja na eneo maarufu la "Beach tope"lililopo Kijichi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI