Mbunge Ulega akitoa maagizo Kwa Diwani dhidi ya Mwalimu mlevi
Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdalah Ulega ameonesha kukerwa na Mwalimu mlevi kupindukia wa shule ya Sekondari Magawa aliyefahamika kwa jina la Edwin Kitaluka anayedaiwa kuwa mzembe kazini kwa ulevi na kumuagiza Afisa Elimu sekondari wilaya ya Mkuranga kufuatilia mienendo yake na kumpatia ripoti ili hatua stahiki ziweze kuchukulia dhidi yake.
Mheshimiwa Ulega ametoa agizo hilo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika Kata ya Magawa kijiji cha Mdimni na kupata malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na Diwani wa Kata hiyo Juma Abeid wakidai kuwa Mwalimu kitaluka analewa kupita kiasi hali inayopelekea kutotekeleza majukumu yake na kusababisha kiwango cha elimu katika shule hiyo kushuka.
Ulega alisema ili maamuzi yaweze kutoka kwa haki bila kuonewa mtu yeyote Afisa Elimu huyo anapaswa kuliangalia swala hilo kwa uangalifu kwa kufuata sheria za kitumishi nakupatiwa taarifa kwa ajili yatua tuazinazofuata.
0 Comments