Na Amon Mtega,_ Songea .
MAAFISA Ugani wanaosimamia shughuli za uzalishaji viumbe maji kutoka Halmashauri za mikoa ya Katavi ,Songwe,Mbeya ,Kigoma na Ruvuma wametakiwa kwenda kuwasimamia na kuwasaidia wafugaji wa samaki ili kuongeza idadi ya Samaki na kisha kumudu soko la walaji.
Wito huo umetolewa na Dkt,Nazael Madalla mkurugenzi idara ya ukuzaji viumbe maji (Samaki)wakati atoa mafunzo kwa maafisa ugani ya namna ya kwenda kuongeza uzalishaji wa Samaki ambayo yamefanyika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Dkt, Madalla amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni Samaki wamepungua kutokana na ongezeko la watu Duniani huku vyanzo vya maji ya asili vikiwa haviongezeki jambo ambalo linasababisha kushindwa kulimudu soko la walaji.
Amesema kufuatia hali hiyo maafisa ugani wanakila sababu ya kuhakikisha wanawsimamia kikamilifu wafugaji wa samaki kwa kuwaelekeza namna ya uchimbaji wa mbwawa pamoja na ulishaji wa chakula kwenye Samaki hao.
Mkurugenzi Madalla amefafanua kuwa kipindi cha nyuma hapa Tanzania mtu mmoja alikuwa anakula Samaki kiasi cha karibu kilo 14 lakini kutokana na ongezeko la watu zimeshuka hadi 8.5 hivyo inatakiwa kutumia fursa ya maji mengine kwa kuchimba mabwawa ili ifikapo mwaka 2025 kila Mtanzania aweze kufikisha kilo japo 10.5 kwa mwaka za ulaji wa Samaki.
Aidha mkurugenzi huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa inatilia mkazo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya uvuvi kwa kuongeza bajeti ya kupanua vituo vingine vya kutotolesha vifaranga vya samaki.
Kwa upande wake mmoja wa wafugaji wa samaki anayetokea mjini Songea Christopher Ndunguru ambaye anadaiwa kuwa na mabwawa 20 amesema kuwa changamoto kubwa ni kutokuwa na kiwanda cha uhakika cha kuchakatia chakula cha Samaki jambo ambalo husababisha uzalishaji kuwa mdogo.
Naye mfugaji mwingine Calvin Challe amesema kuwa licha ya chakula cha Samaki kutokuwepo kwa kiwanda cha uhakika lakini bado hawajapatiwa elimu ya kupambana na wadudu waharibibu kama fisi maji ndege chechengu namna ya kukabiliana nao wasiweze kuwazulu samaki kwenye mabwawa.
Hata hivyo Mfawidhi wa viumbe maji (Samaki) katika kituo cha Ruhila Emmanuel Maneno amesema kuwa kituo kimejipanga kikamilifu kwenye uzalishaji wa vifaranga vya samaki hivyo wakazi wa Mkoa huo waende kwenye kituo hicho.
Pia mgeni rasmi Emmanuel Kisongo ambaye alimuwakilisha katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki awali wakati akifungua mafunzo hayo amesema kuwa suala la ufugaji wa Samaki unaenda kuleta uchumi wa bluu kutokana kuwepo na ongezeko kubwa la walaji .
Kisongo amesema kuwa hivyo mafunzo hayo ni muhimu na kuwa yataenda kuleta mabadiliko katika sekta ya uvuvi ambapo kila mwananchi atafikia malengo ya ulaji wa Samaki.
0 Comments