Na chausiku said, Mwanza
Mkuu wa wilaya ya Magu Salum kalli amesema kuwa mkutano wa Jumuhiya ya pamba ACA unaofanyika jijini Mwanza ni fursa kwa wakulima wa zao hilo kutokana na kujadili mambo mbalimbali yatakayowanufaisha.
Kalli ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano huku akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng, Gabriel Robert na kueleza kuwa mikutano kama hiyo inapojumuhisha mataifa mbalimbali na kuweza kujadili mambo yanayowahusu wakulima wa pamba ni lazima kufikiri zaidi ya hapo na kumuangalia mkulima ananufaikaje na zao hilo.
"Tunapokaa na kujadili mambo ni lazima tujadili mambo ambayo yataweza kuwanufaisha watanzania wanaolima zao la pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mengine ya Tanzania kwa ujumla" Alisema kalli.
Ameeleza kuwa wanahitaji kuona pamba inapata nafasi ya kipekee na inatangaza Tanzania katika ulimwengu wa soko la dunia.
''Sisi kupitia sera iliyowekwa na wizara ya kilimo tutayasimamia haya ili kuhakikisha yanatenda kazi kwa ufasaha" Alisema Kalli.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa bodi ya pamba Tanzania Marco Mtunga amesema kuwa wanahitaji kuchukua hatua madhubiti kama jumhiya ya pamba afrika kwa kuweka nguvu kubwa kwenye utafiti wa teknolojia mbalimbali.
Mtunga ameeleza kuwa kama wakiwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji Soko litapnda na tija katika mazao mbalimbali yatapanda na kuinua uchumi wa nchi.
Mkuu wa chama cha wanunuzi wa pamba Boaz Ogula ameeleza kuwa dhima ya mkutano huo umelenga kuongezeka kwa tija na ubora wa zao hilo jambo ambalo litawapatia mwelekeo mzuri wanunuzi na wakulima kwa sababu mkurugenzi kuu wa bodi ya pamba ameelekeza vitu gani vitafanyika ili kuongezaka kwa tija hiyo.
"Sisi kama wadau mwaka huu tumefarijika sana kwa sababu tumeona serikali imelitambua zao la pamba na kuona ni zao la kimakakati" alisema Ogula
Ogula ameeleza kuwa wizara ya kilimo na bodi ya pamba imefanya jambao la msingi kumtafuta balozi wa pamba na ameweza kufanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wakulima na wameweza kupata elimu namna ya kizingatia upandaji wa zao hilo.
Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya pamba nchini kenya Solomon Odera ameeleza kuwa pamba ni moja ya mazao ambayo yakipewa kipaumbele yanauwezo wa kubadili maisha ya wakulima.
Odera amesema kuwa moja ya vitu vitakavyoweza kufanya wakulima waweze kufukia mafanikio ni pqmojq na ubora wa mbegu ambazo zitawasaidia kupata faida ya biashara wanayoifanya.
"Ukiangalia nchi nyingine zinachangamoto ndio maana tunapokutana tunaangalia sheria kama zinaweza kutusaidia kuboresha zaidi" Alisema Odera.
Mratibu wa utafiti wa zao la pamba Tanzania Tari na Ukirugulu Paul Saidia ameeleza kuwa utafiti wanaoufanya umejikita katika kupambana na changamoto ya zao la pamba katika maeneo mbalimbali kama mkakati wa kuwa na mbegu bora ambayo itakuwa na mavuno na kuwa na ukinzani wa wadudu kama chawajane.
Saidia amesema kuwa katika kupambana na wadudu wasumbufu wa zao la pamba itakayosaidia soko la dunia kukua zaidi.
Aidha ameeleza kuwa mikitano kama hiyo inapofanyika inawasaidia kukitana na watafiti wengine na kuweza kubadilishana uzoefu na kupeana mikakati itakayowasaidia kupambana na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
0 Comments