Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Nchi ya Tanzania imekua ni nchi ya kwanza katika nchi za maziwa makuu kuunda kamati ya kudhibiti mauaji ya kimbari na migogoro katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene wakati alipokua akizungunza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kamati hiyo imefanikiwa kutokana na kuishirikisha Serikali Katika kutatua migogoro ya Kiteto na Mtwara.
Amesema kuwa, lengo la kukutana leo kamati hiyo ni kupanga mipango na kuendeleza mikakati yao, huku ikitarajia kuanzisha ofisi ambayo itaratibu udhibiti wa mauaji ya kimbari na kutatua migogoro.
"Kamati imefanya vizuri sababu imeshirikisha jamii wakiwemo waathirika, watu wanaoheshimika ili kudhibiti matatizo katika jamii yanatatuliwa na jamii yenyewe "amesema Simbachawene.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje, Liberata Mulamula amesema uzinduzi wa kamati ya Taifa inayozuia mauaji ya kimbari ilianzishwa mwaka 2012 .
Amesema kuwa, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi 12 za maziwa makuu na kufanya nchi zingine kuwa na amani kama Tanzania.
"Uswiz inaipa nguvu kamati kutekeleza kuzuia migogoro na mauaji ya kimbari isiweze kutokea katika Kanda, Nchi na Dunia nzima, kamati na wanachama wanatokea sehemu mbalimbali ikiwemo ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri Mkuu na Jeshi la polisi "amesema Mulamula.
0 Comments