Header Ads Widget

MBUNGE PROF PATRICK NDAKIDEMI AKAGUA MRADI WA MAJI KATA YA KIMOCHI

 



NA WILLIUM PAUL,  MOSHI. 

Mbunge wa JIMBO La Moshi  Vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof Patrick Ndakidemi amefanya ziara ya kukagua mradi wa maji kata ya Kimochi unaohudumia vijiji sita.



Mbunge huyo aliyongozana na Diwani wa kata hiyo Ally Badi,  Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu na Mkurugenzi wa MUWSA Mhandisi Kija Limbe pamoja na watendaji wa MUWSA.


Alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwani unahudumia wananchi wa  vijiji sita ambavyo ni Shia, Sango, Mdawi, Mowo, Lyakombila na Kisaseni.


Mbunge huyo alisema kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasani imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa inamaliza tatizo la upatikanaji wa maji linalowakabili wananchi. 


"Niishukuru serikali inayoongozwa  na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za kutatua kero ya maji na miradi mingine iliyopo kwenye Kata ya Kimochi ukiwepo mradi wa ujenzi wa madarasa (5) katika shule ya Sekondari Kimochi yenye thamani ya Shilingi milioni 100 ambazo zilitolewa fedha za UVIKO 19" alisema Prof Ndakidemi. 



Aliongeza kuwa Mradi mwingine mkubwa ni ule wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya Moshi huko Sango uliopatiwa kiasi cha shilingi milioni 979,277,342.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Muwsa, Mhandisi Kija Limbe alieleza kuwa mradi huo wenye thamani ya Tsh milioni 500 unagharamiwa na fedha za UVIKO 19 na unatekelezwa na MUWSA na unategewewa kutatua kero ya uhaba wa maji inayowakabili wananchi waliopo eneo la mradi.


Naye Diwani wa kata hiyo Ally Badi alimshukuru sana mbunge kwa ushirikiano mkubwa uliopo pamoja na kuwashukuru watendaji wote wa MUWSA kwa kazi kubwa wanayofanya katika kata hiyo kuwapatia wananchi maji katika maeneo yao.

Mwisho.... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI