Na Hamida Ramadhan Dodoma
MKUU wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewapongeza wananchi wote wanaolima katika Skimu za serikali huku akiwaonya wananchi hao kuwa Skimu za serikali hazirithiwi wa kurithiswa.
Amesema kumekuwa na shida kwa baadhi ya wananchi kung'ang'ania maeneo ya serikali na kurithishana ndugu zao hali inayoleta Migogoro baina ya wananchi na Serikali .
Amesema katika Wilaya ya Bahi kuna jumla ya Skimu 16 ambazo watu wamekuwa wakizitumia kwa ajili ya kilimo hivyo watambue maeneo hayo sio mali zao ni mali ya Serikali.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati wakati alipowatembelea wananchi wa kijiji cha Mpamatwa, kata ya Mpamatwa Tarafa ya Mpamatwa wilayani bahi baada ya wananchi hao kuandika barua kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana 2021 ya kwamba maeneo yao yanachukuliwa na serikali na kuuzwa kwa mnada bila wao kupewa taarifa yoyote.
Aidha amemtaka Afisa Kilimo wa wilaya ya bahi kusajili kila mtu anayelima katika maeneo yote ya Serikali ili iwe njia sahihi ya kujuana.
" Njia hiyo itakuwa bora kwani wakulima wanaongezeka kila siku huku wengine wakikodisha maeneo hayo sasa niwape taarifa yao tabia hiyo mwisho mwaka huu watu wote mtasajili ili kuepusha migogoro huko baadae,"amesema Mtaka.
Akitatua mgogoro huo amewataka viongozi wa wilaya ya bahi kukaa na kutatau mgogoro baina ya wananchi wa bahi sokoni na wananchi Mpamatwa na akikisisitiza watu wa asili waliokutwa katika eneo hilo wapewe kipaumbele.
Awali akijibu tuhuma hizo za wananchi wa Mpamatwa walioandika barua kwa Rais juu ya kuuzwa kwa maeneo yao Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda amesema nikweli maeneo hayo yameuzwa kwa mnada baada ya wananchi hao kuchukuwa maeneo hayo kwa kipindi kirefu bila kuyaendekeza kwa makusudio husika .
"Sisi hatuna mgogoro ni kweli Mkurugenzi amepima viwanja hivyo nia kubwa ni kukuza mji na ndio maana wameuza maeneo hayo kwa mnada," amesema Mkunda
0 Comments