Header Ads Widget

MAMBO MAZITO KKKT DAYOSISI YA KONDE ,TUME YAAGIZA MAKAO MAKUU YA DAYOSISI KUREJESHWA TUKUYU,ASKOFU AVULIWA JOHO

Mkuu wa KKK Dr Frederick Shoo

Mgogoro uliodumu kwa muda mrefu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde umefikia hatima baada ya Mkuu wa Kanisa hilo Dkt Frederick Shoo kumtangaza Askofu Geofrey Mwakihaba kuwa Askofu mkuu KKKT Dayosisi ya Konde.

Kutangazwa kwa Askofu Mwakihaba kumefuatia uchaguzi uliofanyika leo baada ya Tume iliyoundwa na Dkt Shoo kuja na majibu ya kutokuwa na imani na aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Konde Dkt Edward Mwaikali.

Aidha tume hiyo imetoa mapendekezo ya kurejeshwa kwa makao makuu ya Dayosisi hiyo mjini Tukuyu wilayani Rungwe.

Katika mapendekezo ya tume ya kutokuwa na imani jumla ya kura 204 zilimkataa Askofu Mwaikali na kura 5 pekee ndizo  zilizomkubali.

Askofu Geophrey Mwakihaba  amechaguliwa kuwa Askofu mteule wa Dayosisi ya Konde kwa kupata kura 149 kati ya kura 204.

Mwakihaba anachukua nafasi ya Askofu Edward Mwaikali aliyepigiwa kura za kutokuwa na imani naye.

Pia tume iliyoundwa na Mkuu wa Kanisa Dkt Shoo imetoa mapendekezo kurejesha makao makuu ya Jimbo Tukuyu wilayani Rungwe ambapo pia zilipigwa kura za kutokuwa na imani na aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Dkt Edward Mwaikali huku kura 204 zikimkataa na kura 5 pekee zilimkubali

Matokeo ambayo yametangazwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt Fredrick Shoo.

Kadhalika katika mkutano huo  Dkt Shoo amemtangaza Askofu msaidizi Mchungaji Dkt Meshack Njinga ambaue amepata jumla ya kura 189 ambapo kura 6 ziliharibika na kura 10 zilimkataa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI