Header Ads Widget

KIKWAZO CHA UFAULU CHA WATAHINIWA WA UNUNUZI NA UGAVI NI MASOMO YA HESABU.

 


NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA.


MKURUGEZI Mtendaji wa Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi ametangaza matokeo  ya mitihani ya 23  huku akisema ufaulu  ni asilimia 34.6 huku wastani wa ufaulu kuonekana siyo mzuri .


Akiongea leo jijini Dodoma na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji huyo amesema katika mtihani huo wa 23 walidahili watahiniwa 479 waliweza kufanya mitihani 427  na watahiniwa 28 hawakuweza kufanya mitihani hiyo  kutokana na sababu mbalimbali .


Amesema mitihani hiyo ilifanyika januari  mwaka huu ambapo baada ya kusahishwa na kuchakatwa  kwa mitihani hiyo matokea yalionesha watahiniwa 156 kati ya watahiniwa 451 waliofanya mitihani wamefaulu hiyo ni sawa na asilimia 34.6 ya watahiniwa wote waliofanya mitihani.


 “ Katika Mitihani hiyo watahiniwa 230 watakuwa na mitihani ya marudio baada ya kufaulu somo moja au mawili kwenye masomo yao kwahiyo watapewa nafasi ya kurudia tena masomo yao,’’ amesema Mkurugenzi huyo  .


 Amesema Watahiniwa 65 sawa na 14.4 hao wamefeli na wanatakiwa kurudia masomo yote na watatangaziwa muda wa kurudia masomo hayo.


Hata hivyo amesema kwenye mitihani hiyo kuna mambo yaliojitokeza wamekuwa wakiona mitihani yanayojumuisha mahesabu mambo ya takwimu na uchumi kumekuwa na tabi ya watahiniwa kufeli lakini katika mitihani hiyo ya 23 masomo taaluma yanayohusu  ununuzi na ugavi  watahiniwa wamefeli sasa hiyo ni changamoto kwani hayo ndio maeneo yao watakayoenda kufanyia kazi.


“ Kitendo cha kufeli kiasi hicho kinaipa bodi  jukumu la kuweka mikakati ya kuhakikisha watahiniwa wanaelewa wanacho fundishwa na kuweza kufauli vizuri mitihani yao,” amesema . 


Pia amesema wamaejaribu kuangalia katika masomo yote watahiniwa walifanya masomo 32 masomo 6 waatahiiwa walifanya vibaya na masomo 17 walifaulu wastani  na masomo yalibaki walifanya vizuri kiasi chake kwahiyo ufauru 34.6 kwajumla matokeo si mazuri .


Bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi imeweka mikakati ya kuwasaidia watahiniwa wao kwa kuhakikisha vituo vyao vya kujiandaa na mitihani vinasimamiwa vizuri vikiwa na walimu wanao fundisha na wenye uwezo pamoja sifa stahiki ili kuboresha  uelewa wa wanafunzi wanapokuwa vyuoni na hatimaye uelewa huo uweze kuwasaidia wanapokuja kufanya mitihani ya kitaaluma.


“Kitendo cha kutangazwa kwa matokeo hayo   sasa Wanatangaza  mitihani ya 24  waanze kujisajili na usajili unafanya kwanjia ya mtandao  hivyo waje kujisajili nawale wanaotakiwa kurudia mitihani wajiandae kwa mitihani hiyo”. Alisema.


Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi  ni tasisi iliyopo chini ya wizara ya fedha na mipango iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 23 mwaka 2007 kwaajili ya kusimamia  tasnia nzima ya ununuzi na ugavi hapa nchini.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI