Teddy Kilanga _Arusha
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Elirehema Kaaya amezitaka halmashauri zote nchini kuachana na tabia ya ujenzi wa kusambaza majengo mengi katika eneo moja na badala yake kuanza ujenzi wa magorofa ili kuendana na thamani ya bei za viwanja .
Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ambayo amekuwa akifanya katika halmashauri mbalimbali ambapo alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Arusha pamoja na hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha na kuonesha kulizika na matumizi ya fedha za Serikali .
Katibu huyo alisema hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ta Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika mkutano uliofanyika Jijini Dodoma na ambapo aliwaagiza ALAT kufuatilia fedha zinazotolewa katika halmashauri na kubaini matumizi yake .
"Nimefarijika leo nimepata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ya Arusha ambapo nimejionea kazi nzuri zilizofanyika ikiwa halmashauri ya jiji la Arusha ilipokea kiasi cha sh.bilioni 2.1 nakufanikiwa kujenga vyumba 105,"alisema Kaaya.
Aidha alipongeza halmashauri hiyo kwa matumizi mazuri ya fedha hivyo anaungana na Waziri Mkuu kupongeza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini pamoja na wakuu wa mikoa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi).
Pia alimpongeza Mwenyekiti wa halmashuri ya jiji la Arusha,Maximilan Iranqe pamoja na Mkurugenzi John Pima,wataalamu na baraza la madiwani la jiji hilo kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa miradi mbalimbali katika kufuata vigezo na masharti ya serikali.
"Naendelea kutoa wito katika halmashauri zote nchini kwani thamani ya viwanja kwenye maeneo ya mijini huwa ni kubwa sana hivyo muendeleze na muundo wa majengo ya ghorofa katika shule zetu hizi kwani husaidia kupata nafasi za kiwanja tulivyonavyo kwa kutandaza majengo humaliza eneo,"alisema.
Kaaya alisema muundo wa maghorofa sio kwa shule pekee hata majengo ya afya hutakiwa hivyo kwa kuangalia jiji la Arusha lipo na utofuti kidogo wa kimkakati ukiangalia mpakani Namanga watu wanaendesha biashara zao kupitia kenya,pia suala la utalii kupitia mbuga za wanyama ikiwemo Ngorongoro na ndio sababu iliyopelekea ujenzi wa hospitali ya kitalii.
Kwaupande wake Mwakilishi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Jiji la Arusha Nuraji Msuya alisema baada ya miundombinu ya hospitali hiyo ya wilaya ya Arusha kukamilika wanafanya kazi bila changamoto yoyote.
Huku baadhi ya wananchi katika Jiji hilo walipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha huduma mbalimbali katika Jiji hilo ambapo hapo awali walikuwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Rais Samia alitangaza kupokea shillingi Tirion 1.3 kutoka bank kuu ya dunia ambapo zilitolewa kwaajili ya kumaliza changamoto ya upunguza wa vyumba vya madarasa 12000 na ili kuhakikisha changamato hiyo inamalizika kabisa walijenga vyumba 15000 ambapo Halmashauri ya Jiji la Arusha ilipata kiasi cha shillingi bilioni 2.1 na kujenga vyumba vya madarasa 105 .
0 Comments