.
Na,Jusline Marco;Arusha
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na kushirikiana ili kulinda matumizi sahihi ya rasilimali za umma.
Kichere ameyasema hayo wakati akizungumza na menejimenti ya Ngorongoro, ambapo amesema njia pekee ya taasisi kufanya vizuri pale zinapokaguliwa ni kuzingatia sheria,Kanuni na taratibu zilizowekwa.
“Siku zote mnapotimiza majukumu yenu ya kila siku ni muhimu kuzingatia sheria, weledi na kukumbuka kuwa mpo ili kuwatumikia watanzania kupitia rasilimali mnazosimamia”,alisema bwana Kichere.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru mbali na kumpongeza CAG kwa ziara hiyo, amesema kuwa mamlaka itaendelea kuboresha mifumo utendaji kazi hususani kusimamia kikamilifu shughuli za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii ili kuendelea kuongeza tija kwa Taifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.
0 Comments