Header Ads Widget

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAITAKA TAEC KUPANUA WIGO WA UTOAJI WA ELIMU

 


Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu  ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii , Aloyce Kamamba ameitaka Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kujikita katika utoaji wa mafunzo ya udhibiti mionzi katika hospitali ,ofisi na hata mashuleni ili kuweza kudhibiti tatizo la mionzi lisilete madhara kwa watumiaji hao.Mwandishi Teddy,MDTV  Kilanga

 Aidha ameitaka TAEC kuongeza upana wa uwezeshaji wa udhibiti mionzi na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi  badala ya kujikita mipakani tu .

Akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea tume hiyo katika kujionea  shughuli na miradi mbalimbali inayofanyika ambapo wamefurahisha na utendaji wa tume hiyo.

Kamamba amesema kuwa, pamoja na kuwa wamejikita zaidi katika maeneo ya mipakani ni vizuri wakapanua wigo zaidi na kuweza kuwafikia wananchi wengi  na kuweza kufahamu huduma zinazotolewa na tume hiyo .

"Kwa kweli tumetembelea na kujionea mradi mkubwa wa maabara unaotekelezwa hapa na tumeridhishwa na mradi huu  ,na tumeona mradi unatekelezwa ndani ya mda na tupo tayari  kutoa ushirikiano wa kutosha ili kutimiza  majukumu yao kwa ubora zaidi "amesema.

Hata hivyo aliishauri  tume hiyo kuangalia namna ya kudhibiti mbu wanaoeneza malaria kama walivyofanikiwa kudhibiti mbung'o  Zanzibar .

Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Tume hiyo,Prof.Lazaro Busagala amesema kuwa, chuo hicho  kimefanikiwa kutoa elimu kwa shule 50 za sekondari ambapo wanaendelea na shule zingine lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu kuhusu na maswala ya mionzi na athari zake .

Amesema kuwa, wamejipanga kwenda kutoa elimu serikali za mitaa ili kuleta maendeleo yanayohitajika katika nchi na kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali.

Prof .Busagala amesema kuwa,TAEC iliingia mkataba na wakala wa ujenzi Tanzania (TBA) kwa ajili ya ujenzi wa maabara awamu ya kwanza mei 29 ,2017 ambapo ulikamilika april 29,2018 na  hadi kukamilika kwake ujenzi huo uligharimu shs 2.3 bilioni.

Amesema kuwa, Tume hiyo iliingia mkataba na kampuni ya china ya LI JUN Development contruction co ltd kwa ajili ya ujenzi wa maabara awamu ya pili septemba 10,2019 mkataba wa miaka mitatu ambao una thamani ya shs 10.4 bilioni ,ambapo hadi kufikia machi 9,2022 ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 94 ambapo upo mbele kwa miezi mitatu ukilinganisha na mpango kazi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Mwanakwerekwe Zanzibar ,Kassim Haji alishauri Tume hiyo kuharakisha utoaji mafunzo kwa vyuo, pamoja na mashuleni ili waweze kuipata elimu hiyo wakiwa tangu wadogo na kuweza kuifahamu tume hiyo na kujua athari zitokanazo na mionzi na kuweza kuchukua hatua za haraka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI