Teddy Kilanga_Arusha.
Kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria imeridhizishwa na ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki Arusha nakuwaomba watendaji wake kutumia miundombinu hiyo kutoa haki kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Wakizungumza baada ya kutembelea kituo jumuishi cha utoaji haki mkoani Arusha kwa nyakati tofauti baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo,wamesema kutokana na ubora wa kituo hicho ikiwemo miundombinu bora iliyojengwa hivyo ni vyema wakazingatia kuweka matangazo yanayopita katika televisheni katika kuta za mahakama juu ya kesi ili wananchi waweze kuelewa.
Mbunge wa jimbo la Mahonda kaskazini Unguja,Abdullah Mwinyi amesema pamoja na kituo hicho cha utoaji haki mkoani Arusha kujengwa kwa ubora pia wamezingatia mila na desturi za kitanzania kwa kwani alama zinasehemu yake katika kuwakilisha utamaduni wa nchi.
"Naomba ni nipongeze zaidi ujenzi wa vituo hivi kwani umezingatia nyanja mbalimbali ikiwemo chumba cha wanawake kunyonyeshea mtoto kwani katika nchi za wenzetu utamaduni wa kunyonyeshea hadharani haupo,"amesema Suma Ikenda Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya.
Pia Mbunge wa viti maalum upande wa watu wenye mahitaji maalumu mkoa wa Dodoma,Khadija Shabani amesema kupitia ujenzi wa kituo hicho ni vyema ofisi nyingine zikaiga mfano wa ujenzi huo ili kuwarahisishia wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma pamoja na kuokoa gharama.
Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo,Emmanuel Mwakasaka amesema miundombinu ya kituo hicho jumuishi mkoani Arusha mazingira yake yanaridhisha kwani mazingira hayo ni tofauti na magereza hivyo ni vyema magereza pia yakaboreshwa ili yaweze kuendana na kituo hicho.
Kwa upande wake Mtendaji wa mahakama kuu ya Tanzania,Prof.Elisante Ole Gabriel amesema wanamalengo ya kujenga vituo jumuishi vya utoaji haki 12 na mahakama za mwanzo 60 ambapo manufaa yake ni kuongeza imani ya mahakama kwa wananchi.
"Kwa sasa kituo hiki kinawasaidia wananchi katika kuokoa muda kutokana na uwepo wa mahakama zote kuwepo katika kituo hiki jumuishi pia inaepusha mrundikano na kuongeza hari ya utendaji,"amesema Prof.Gabriel.
Aidha amesema kuwa watatunza miundombinu hiyo na rasilimali zilizopo kwa ajili ya kizaji kijacho vilevile wanatumia mnyororo wa Tehama katika kuhakikisha wanaongeza tija katika hutoaji wa huduma kwa haki kwa kuhakikisha wanapata kile kilichokusudiwa.
Naibu waziri wa katiba na sheria,Geofrey Mizengopinda amesema nchini kuna vituo jumuishi sita ambapo wanahitaji vifikie 12 ili wawapungizie adha watanzania ambao wanahitaji kupata huduma hiyo bila kutumia gharama kubwa.
"Na umejidhihirisha kwenye hili jengo linasaidia wananchi kupata huduma zote za utoaji haki ikiwemo huduma za msaada wa kisheria ambazo kimsingi walikuwa hawapati katika muundo ule wa awali wa mahakama moja ikiwa hata majengo hayakuwa rafiki lakini kwa sasa tunaelekea kwenye ukweli kuhusu maisha,"amesema Pinda.
0 Comments