![]() |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda |
Na. Andrew Chale,
TAMASHA kubwa la kukuza uchumi wa Blue kupitia sekta ya Uvuvi na Utalii Bagamoyo Mkoani Pwani la Samaki Festival limezunduliwa rasmi asubuhi tarere 21,Juni 2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda kwa shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo usafi maeneo ya fukwe, michezo ya ufukweni na elimu sahihi ya uvuvi kwa wadau wa uvuvi.
Katika tukio hilo, Mkurugenzi amewataka wadau wa uvuvi kuzingatia usalama wao pamoja na masuala ya usafi ikiwemo kulinda bahari ambapo nae ameweza kushiriki kufanya usafi na wananchi na vikundi vya michezo waliojitokeza.
Aidha, tukio hilo jioni linaendelea katika eneo la Ikulu ya Mjerumani Old Boma kwa burudani mbali mbali na matukio ya biashara ikiwemo samaki na bidhaa zingine zitaendelea kuuzwa.
Clara Premsingh, Mkurugenzi wa Creators Hub, amesema mbali na matukio hayo ya asubuhi, jioni Samaki Festival ni burudani kemkem kutoka kwa wasanii wa ndani ya Bagamoyo na nje, Wasanii wa Singeli na vikundi mbalimbali vya burudani vitakavyopiga muziki wa 'live' watachangamsha tamasha hilo.
"Wakazi wote mnakaribishwa hakuna kiingilio. Wasanii nyota wa Singeli kama Virus Mdudu pamoja na wengine watakuwepo.
![]() |
Clara Premsingh, Mkurugenzi wa Creators Hub akizungumza katika tukio hilo |
Pia waåp Wasanii wengine kama, Timitee, The Birds, Dartone Mnyama, Welle, Micky Singer, Safari Rockers ambapo hao watapiga muziki wa moja kwa moja wa bendi "Live Band," na Wasanii wengine ni Dogo Zero na wenzake ambao wao watapiga singeli (playback).
Aidha, amesema Samaki Festival ni la kipekee na Wana Bagamoyo na viunga vyake pamoja na majirani zake Dar Es Salaam watafurahia tamasha hilo.
Clara amesisitiza kuwa, wadau watafurahia tamasha hilo kwani pia Ulinzi umeinarishwa wa kutosha kutoka kwa Jeshi la Polisi Bagamoyo na kampuni ya SGA.
0 Comments