Header Ads Widget

JUVIMA - TUNATAKA KATIBA MPYA, TUME HURU SIO KIPAUMBELE CHETU

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Jumuiya ya Vijana wa Mageuzi (JUVIMA) wameitaka Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza mchakato wa katiba mpya haraka iwezekanavyo kutoka kwenye rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba mpya ya Jaji Joseph Warioba na wenzake kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.


Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa JUVIMA Nicolas J. Clinton wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema katiba mpya ndio jawabu la changamoto zote zinazowakabili watanzania ikiwemo kiuchumi, kisiasa pamoja na kijamii.


Amesema kuwa, kipaumbele cha Juvima ni kudai katiba mpya na sio tume huru kama wengine, kwani wao wanaamini endapo itapatikana katiba mpya, lazima itazaliwa na tume huru, hivyo wamejipanga kuunganisha nguvu kwa vijana wote katika kudai katiba mpya.


Amesema kuwa, takwa la jamii ya watanzania walio wengi tangu Serikali ya awamu ya pili ya mzee Ali Hassan Mwinyi ni katiba mpya, hivyo Juvima inaungana na watanzania wote kudai katiba mpya usiku na mchana, huku akieleza uhai wa nchi hiyo upo kwenye mikono ya katiba mpya na sio kikosi kazi .


Ameongeza kuwa, katiba iliopo kwa sasa pamoja na mambo mengine ni katiba ya chama kimoja ambapo inakijenga, kukulinda na kukipendelea licha ya kuwa katiba hiyo inatambua mfumo wa vyama vingi, hivyo wamejipanga kudai katiba mpya kwa hali yoyote ile.


"Mahakama na bunge vimekua vikibemendwa na Serikali ya CCM na vinafanya kazi kama Taasisi za chama tawala, tunataka kubadili mfumo mzima wa kuendesha nchi yetu na tayari kuna maoni ya wananchi kupitia tume ya mabadiliko ya katiba ya Jaji Warioba na wenzake"amesema Nicolas.


Hata hivyo, amesema kutokana na katiba iliyopo sasa haikidhi mahitaji ya watanzania, ni lazima kuanzia sasa kuidai na wala hawatasubiri mpaka mwaka 2025 au baada ya hapo huku akieleza juhudi za kukwamisha  mabadiliko ya katiba mpya zitashindwa.


Aidha, amesema wataunganisha nguvu ya Vijana wa Nchi nzima bila kujali itikadi, dini,  kabila wala rangi zao kwa kuwa katiba ya nchi ni ya watanzania wote Ili kuhakikisha wanajua umuhimu wa katiba mpya kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI