Header Ads Widget

HERI JINO MOJA KULIKO KIBOGOYO

 


Adeladius Makwega- DODOMA


Siasa za Tanzania yetu zimekuwa zikifanyika zikiwa na mambo mengi ndani yake, huku  baadhi ya watu wakidhani kuwa ili kuweza kushiriki siasa za taifa hili zikihitaji tu mtu huyu kuwa na ujuzi wa kuongea tu wakati jambo hilo si kweli.


Uchaguzi umekuwa ukihusianisha mambo mengi mno ikiwamo kabila la mgombea, nasaba yake, aina za alama, ukanda wa mhusika  hata kama hayasemwi hadharani lakini kwa sehemu kubwa yana ushawishi mkubwa.


Mwaka 1965 katika jimbo la Shinyanga ndugu John Rupia ambaye alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara maarufu wa Tanzania tangu enzi za Tanganyika ambaye awali alikuwa mbunge wa jimbo hilo alishindwa Uchaguzi Mkuu katika jimbo hilo.


John Rupia alishindwa na mwanasaisa Bakari Msonde ambaye alikuwa mwanasiasa asiye mzungumzaji aliyekulia Tanga huku akiwa na asili ya Shinyanga. Inadaiwa kuwa hakuwa na mwanasiasa mzuri na alikuwa na  wasifu mdogo .


Katika jimbo hilo hilo mwaka 1970 kulifanyika uchaguzi Mkuu naye Mwandu Luhanya ambaye alikuwa mwnasiasa maaraufu ambaye alikuwa na fedha mno huku akifahamika na wengi lakini alishindwa katika uchaguzi huo na Anna Tito Kulwa ambaye hakuwa akifahamika mno.


”KIlichosababisha John Rupia na Mwandu Luhanga kushindwa katika chaguzi hizo za 1965 na 1970 wengine wakidai kuwa ni ishara walizotumia katika uchaguzi huo ambazo ni nyumba huku wagombea wenzao walitumia jembe na kushinda.” 


Anasema D Kang’wenzi katika utafiti wake juu ya imani ya jembe kwa kabila la wasukuma huko Shinyanga na matumiziya ishara katika  siasa.


Ndiyo maana Chama cha Mapinduzi CCM kilipoundwa mwaka 1977 kiliamua matumizi ya baadhi ya ishara kwa chama chake kwani kisiasa walibaini kuwa hilo lina maana kubwa kwa jamii ndan ya majukwaa ya siasa.


Awali siasa zilifanyika hivyo lakini kubwa na la msingi kwa sasa kisiasa ni ile tafsiri ya vitendo ya ile mipango ya vyama vya kisiasa kwa jamii. Kama ni jambe hilo la mkulima ni ile mipango yake ya kilimo kwa wakulima kama kupatikana kwa zana bora za kilimo, mbegu bora na mbolea kwa wepesi.


Mwaka huo huo 1965 ulikuwa mwaka wa uchaguzi, lakini kwa maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 1970 kulitenganishwa mipaka ya majimbo baina ya Kusini na kaskazini wilayani Kahama. Baadae ikawa Kahama Mashariki na Kahama Magharibi. Mabadiliko yalifanyika tena Kahama Kusini (Dakama) na Kahama Kaskazini(Msalala).


Mgawanyo huo ulilenga mgao wa idadi ya watu hili kila jimbo liwe na idadi ya watu sahihi kwa mahitaji ya jimbo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati huo iliomba ushauri kwa viongozi wa TANU akiwamo mwenyekiti na katibu wake.


“Mara baada ya mgawanyo huo ilibainika kuwa Wanyamwezi wengi waliwekwa upande wa jimbo la Dakama huku Wasumbwa na Wasukuma waliangukia jimbo la Msalala. Maamuzi haya yalikuwa na changamoto kubwa katika uchaguzi wa mwaka 1970 na maendeleo ya eneo hilo.”


Haya yanasemwa na V Mlekwa katika utafiti wake wa wilaya ya Kahama na changamoto za maendeleo mwaka 1973.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya wakati huo ilitoa nafasi ya wapiga kura kujiandikisha mpaka Julai 15, 1970 katika Wliaya ya Kahama karibu wapiga kura 67,201 walishajiandisha kuanzia Julai 1- hadi 15, 1970 kwa muda wa ziada wapiga kura 5000 wa ziada walijiandikisha.


Ndiyo kusema kwa hesabu ya namba ilikuwa mpaka Julai 15, 1970 Jimbo la Dakama wapiga kura 33,909 walijiandikisha na kwa jimbo la Msalala wapiga kura 33,293 walijiandikisha. Hii ilitoa picha ya wapiga kura asilimia 85 walijiandikisha kushiriki uchaguzi huo, nayo ilikuwa ni asilimia 85 ya  wananchi wote wenye sifa hiyo kwa wilaya ya Kahama.

Ilibainika kuwa wastani wa waliojiandikisha kitaifa kwa mwaka 1970 ilikuwa ni asilimia 74 kwa nakisi (tofauti) ya asilimia 11 (85-74).


Ifahamike wazi kuwa wakati huo vyama vingi vilishafutwa, chama kilichokuwa kinatawala kilikuwa ni TANU huku kikiendelea na siasa za uchaguzi wa ndani ilikupata wagombea wake kwa ngazi ya majimbo.


Agosti 12, 1970 wajumbe 319 wa TANU walitakiwa kukutani na kupiga kura za kupendekeza majina ya wagombea Ubunge kwa majimbo hayo huku wajumbe 295 wakifika ukumbini.


Hapa kila tawi la vijijini lilipata nafasi ya wapiga kura 10 walati awali kila tawi lilikuwa naw ajumbe wawili wenye sifa. Msalala matawi 12 na Dakama wajumbe 9.


Ndiyo kusema Msalala ikiwa na wajumbe wengi zaidi ya Dakama. Wakati uchaguzi huo ambapo wajumbe wote walipiga kura pamoja Kiwilaya bila ya kujalia jimbo. Mwenyekiti wa uchaguzi huo aliwaomba wajumbe kuwa japokuwa walikaa mjini kwa siku mbili bila ya kupatiwa posho zao lakini wasijikisie vibaya kwani hiyo ni mojawpao ya majukumu ya viongozi kwani kubwa ambalo lililo mbele yao ni ujenzi wa taifa.


“Wajumbe hao walihakikishiwa kupata haki zao baada ya uchaguzi huo.” 


Kumbe mwanakwetu wajumbe walikuwa makini kwa haki zao kitambo sana.


Katika uchaguzi huo kulikuwa na wagombea 20 kiwilaya. Kwa Jimbo la Msalala ndani ya uchaguzi wa TANU ndugu Thadeo Ndazi alipata kura 102 akifuatiwa na ndugu Rashidi Nassoro aliyepata kura 43. Naye Lumelezi Mganga alipata kura 37 na Nzumbi Michael Nkwabi alipata kura 30.


Kwa jimbo la Dakama Ndugu Maganga Msanja Shija alipata kura 77 akifuatiwa na Edward Maiga Msoma Maige aliyepata kura 62 Fares Mahoga Lukinga alipata kura 59.


NEC ya TANU ilifanya maamuzi kwa jimbo la Msalala walimteua ndugu Rashidi Nassoro na ndugu Zumbi Michael Nkwambi kugombea jimbo hilo maana chama cha TANU kilikuwa na wagombea wawili ambao ndiyo walioshindana katika jimbo hilo. Wakati alieshinda mbele ya wajumbe ni ndugu Thadeo Ndazi huku jina lake likitupiliwa mbali.



Maamuzi haya ya NEC ya TANU yalimuweka kando ndugu Lumeleze Adam Mganga ambaye alikuwa watatu kwenye kura za wajumbe ambaye aliwahi kugombea ubunge kwa jimbo la Kahama Magharibi na kushindwa mwaka 1965, na ndugu Fares Mahenga Lukinga. Huku hawa wagombea wawili waliotupwa pembeni wakiwa na sifa zinazofanana, likiwamo kabila la Wasumbwa.


Haikufahamika kama NEC ya TANU ilitilia maanani jambo hilo. Pengine hilo lingesababisha ndugu Adam Lumeleza Mganga angeshindwa uchaguzi tena.


Nako katika jimbo la Dakama NEC ya TANU iliamua kuwachagua ndugu Lukinga ambaye alikuwa watatu naye ndugu Masanja Shija aliyekuwa wakwanza akitupiliwa mbali.  Haikufahamika kwanini NEC ya TANU walimteua ndugu huyo.


Ndani ya uchaguzi mkuu jimbo la Msalala, ndugu Mzumbi alipata kura 14,518 na ndugu Nassoro alipata kura 8471 nalo Jimbo la Dakama Ndugu Lukinga alipata kura 14,026 na ndugu Shija alipata kura 6368.


Kwa hakika kisiasa ni jambo jepesi sana kuweza kufanya ujanja kwa kundi dogo la wajumbe kuliko kwa kundi kubwa la wapiga kura 


Pia ifahamike wazi kuwa kwa maamuzi ya NEC ya TANU kwa Jimbo la Msalala kwa wagombea Nzumbi na Nassoro na kwa jimbo la Dakama kwa wagombea Shija na Dakama maafisa wa TANU  chini ya Julius Nyerere na maamuzi ya wapiga kura yana mambo mengi. 


Kama walivyokuwa NEC ya TANU walivyotazama mengi kawa majimbo haya na wao wapiga kura walitazama mengi. Kama NEC ya TANU ilipiga hesabu zake nao wapiga kura wa uchaguzi mkuu huo kwa majimbo ya Msalala na Dakama walipiga hesabu zao, hayo ni mahesabu ya kisiasa.

Hiyo ni kwa hali ya chama kimoja, je hali ikoje panapofanyika uchaguzi wa vyama vingi?


Hata maoni ya wapiga kura katika uchaguzi huo walidiriki kusema.


“Heri kumchagua MWENYE JINO MOJA kuliko kumchagua KIBOGOYO.”


makwadeldaius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI