Header Ads Widget

WAZIRI WA ELIMU PROF MKENDA AGAWA KOMPYUTA 300 KWA VYUO VYA UALIMU

  


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amegawa jumla ya Kompyuta 300 kwa vyuo vya ualimu  huku akisema mgao huo umezingatia  uwiano kati ya wanachua na vifaa vilivyopo katika vyuo kwa sasa.Mwandishi Hamida Ramadhan Dodoma


Ameyasema hayo leo jijini hapa wakati akikabidhi Kompyuta kwa vyuo vya ualimu Kompyuta  za Mezani na Kompyuta Mpakato ambapo Amesema  Jumla ya Kompyuta 300 zitakazogaiwa kwa vyuo 13. Vyuo 4 vitapata Kompyuta 30 na Vyuo 09 Kompyuta 20. 


Aidha, vyuo vyote 35 vitapatiwa Kompyuta Mpakato 1 kwa ajili ya kusaidia idara

zenu vyuoni.


" Kompyuta hizi zimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo naagiza kila Mkuu

wa Chuo kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengo ya kuimarisha

ufundishaji na ujifunzaji Chuoni," amesema Waziri Mkenda 


Hata hivyo amewataka Kila Mkuu wa Chuo kuhakikishe mali zote

za Serikali zinatunzwa ipasavyo ili kuleta tija ya fedha zilizotumika vyuo

vyote vya Ualimu vizingatie matumizi sahihi ya kompyuta hizi ikiwemo kuhaikikisha ziko katika mazingira yaliyo safi na salama kama ilivyo kanuni

na taratibu za kutunza na kuhifadhi vitu vyaTEHAMA.



"Mtakumbuka kuwa, Wizara imekwisha gawa vifaa vya TEHAMA ikiwa ni

Kompyuta za Mezani (Desktop) 1,120, Kompyuta za mkononi au

Kompyuta Mpakato (laptop) 113, na Projekta 186," amesema  Waziri Mkenda 


Ameeleza  kuwa Vifaa hivi viligawiwa kwa Vyuo vyote 35 vya Ualimu, hivyo vifaa vya leo ni nyongeza ili kukidhi

mahitaji. Hii itasaidia kupunguza uwiano wa matumizi ya kompyuta kwa

Wanachuo kutoka Wanachuo 28 kwa Kompyuta 1 (28 :1) hadi kufikia

Wanachuo 2 kwa Kompyuta 1 (2 :1) vyuoni.


Amesema wa matumizi ya vifaa na mifumo hiyo ya TEHAMA iliyoboreshwa inahitaji pia kuwepo kwa Mtandao imara, hivyo, Wizara itaviunganisha Vyuo vyote

vya ualimu katika Mkongo wa Taifa ili kuhakikisha kuwa Vyuo vinaweza

kupata mtandao imara utakaowawezesha Wakufunzi na wanachuo kutumia ufundishaji na ujifunzaji kwa ufanisi. 


" Kwa mwaka huu tunatarajia

kuunganisha Vyuo 15 vya Ualimu katika Mkongo wa Taifa Kazi ya

Kuunganisha Vyuo hivyo inaanza leo tarehe 21/02/2022 baada ya Wizara

kuwakabidhi wakandarasi wawili (BM Telecommunication na SoftNET

Solution)," amesema 


Awali akisoma taarifa ya  Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP) Kaimu Katibu Mkuu wizara ya Elimu Caroline Nombo amesema mradi namba 4323 katika horodha ya mradi inayotekelezwa na serikali mradi unatekelezwa  kwa ushirikiano kati ya serikali ya jamhuri ya ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu na serikali ya Canada kupitia ubalozi wake hapa nchini.


Amesema Mchango wa serikali ya Canada katika mradi huo ni jumla ya Dola za KiCanada shilingi milioni 53 mchango wa serikali ya Tanzania ni kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa vyuo zikiwemo gharama za malipo ya chakula kwanavyuo na gharama zamafuzo ya vitendo kwa walimu .


"Dhumuni kuu la mradi huu ni kuendekeza elimu ya ualimu hapa nchini kwa kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji wanufaika wa mradi huo ni vyuo vyote vya serikali 35 ofisi ya tamisemi taasisi ya elimu tanzania baraza la mitihani tanzania wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu," amesema Kaimu katibu mkuu huyo


Malengo kuimalisha miundombinu  na mifumo ya tehama katika vyuo vyote vya ualimu 35.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI