Header Ads Widget

WAZIRI NDUMBARO AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA UTALII NA UWINDAJI



WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro amewataka wawekezaji katika Sekta ya Utalii na uwindaji kufuata sheria za mikataba yao sambamba na kuondoa mikwaruzano .Mwandishi Hamida Ramadhan MDTV Dodoma


Amesema Mikwaruzo hiyo ni baina ya makampuni hayo kwani uhasama huo unafifisha juhudi za Serikali katika kuendeleza utalii.


Dkt Ndumbaro ametoa wito huo jijini hapa wakati alipokutana na makampuni ya uwindaji yaliyoshiriki katika mnada wa vitalu vya uwindaji mnada uliofanyika Januari 2022 huku akisikiliza malalamiko yao kwaajili ya kuyatatua ili kuondoa Migogoro.


"Serikali imekuwa ikiondoa vikwazo mbalimbali ili kuinua sekta hiyo na kuhakikisha inanufaisha taifa kwa kuongeza pato la Taifa na fedha za kigeni," amesema Dkt Ndumbaro


Kwaupande wake Muwakilishi wa wenye makampuni ya uwindaji bwana Akiram Azizi kutoka kampuni ya kilombero North ni miongoni mwa wawekezaji ambao malalamiko yao yamesikilizwa huku Waziri akiahidi kuyatolea maamuzi Februari 16 Mwaka huu baada ya kuyafanyia kazi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI