Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI SABA WAKAMATWA TANGA

 


WAANDISHI wa habari saba mkoani Tanga wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi wakati walipokuwa wakizungumza na mashabiki wa timu ya Costal Union walikuwa wakilalamikia uongozi wa timu hiyo.


Waandishi hao Mariam Shedafa wa Azam Tv,Alex Abrahamu wa Habari Moto Blog ,Boniphace  Gideoni wa Nipashe ,Absalum Daudi mpiga picha wa Azam  Hadija Bagasha wa East Africa Ibrahimu  Kunoga wa Global Tv na Denis Chambi wa Championi..


Waandishi hao walikamatwa katika viwanja vya  Popatlal mahali ambapo timu hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi.


Wamesema hawajui sababu ya kuwekwa ndani wakati walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya kitaaluma.


Waliongeza kuwa kitendo cha kuwekwa ndani kwenye kituo cha polisi Chumbageni kwa saa tatu kimefanya jamii kutohabarishwa kile kilichokuwa kikiendelea kwa mashabiki wa timu ya Costal Union.


Kuhusu vifaa vyao walisema  walinyanganywa kila kitu ikiwemo simu  kamera  huku wakisachiwa kwenye mabegi yao  kubaini  vifaa vyote vilivyotumika kurekodi.


Kwenye mabago yaliyokuwa yamebebwa na wahabiki wa timu hiyo yalikuwa na jumbe mbalimbali za kulalamikia viongozi wa timu hiyo akiwemo kocha wake Melis Medo wakionesha kulaami kitendo cha timu hiyo kufungwa mechi nne  kwenye michuano ya ligi kuu.


Kwenye mabango hayo walamlalamikia mwenyekiti wao club hiyo Stephen Mguto kwa kushindwa kuienesha club hiyo.


Waandishi hao waliachiliwa kwa nmashariti ya kutoandika na kusambaza habari hiyo kwenye vyombo vyao.


Mwenyekiti wa Club hiyo Stephen Mguto alisema haoni mahali timu hiyo imeshindwa kufanya vizuri.


Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Lulu George alilaani kitendo cha waandishi wa habari kukamatwa wakiwa wanatekeleza majukumu yao  katika viwanja vya Popatlal  jijini Tanga.


Lulu alionesha kushangazwa na vitendo vya aina hiyo  na kusema kuwa ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na kukiuka haki  zawaandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao.


Lulu aliviomba vyovyo vya dola kuwalinda waandishi wa habari wakiwa wanatekeleza majukumu yao badala ya kuwakamata na kuwatia hofu ya kuihabarisha jamii mambo yanayoendelea kwenye maeneo yao na nchi yao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI