WANAFUNZI 18 wa shule ya msingi Nyololo katika Wikaya ya Mufindi mkoani Iringa, wamelalamikia kufanyiwa ukatili wakingono na mwalimu wao wakiwa shuleni, tukio linalotajwa kuzua maswali yasiyo na majawabu.Mwandishi Oliver Motto anaripoti toka Mufindi
Wakizungumzia mkasa huo wakikatili wa kingono unaotajwa kutekelezwa na mtuhumiwa anayedaiwa kuwa ni mwalimu wao, wanafunzi hao wamesema kwa nyakati tofauti Mwalimu huo amekuwa akiwaita katika maktaba na kuwakamata kinguvu, na kuwavua sketi na nguo za ndani na kisha kuwaingiza vidole katika sehemu za siri.
Wanafunzi wengine wamesema Mwalimu huyo waliyemtaja kwa jina moja la Mtanga huwaita mmoja mmoja ofisini akiwaraghai kuwa anawasahihishia madaftari, na baada ya kufika huko huwakamata kinguvu na kuvuliwa Sketi na kisha kutekeleza ukatili huo wa kuwaingiza vidole katika sehemu za siri za mbele na nyuma za wanafunzi hao wa kike.
Aidha walisema mwalimu huyo huwafanyia ukatili huo muda wa jioni wanapokuwa wamebaki kwa masomo ya ziada, na pia siku za wikiendi kama jumamosi, na hufanikisha unyama huo kutokana na yeye kuishi eneo jirani na shule hiyo.
Pia wamesema huwavizia walimu wenzie wakiwa wameondoka na yeye kurudi shuleni hapo kwa madai kuwa anataka kuwafundisha masomo likiwemo la hesabu, na ndipo humuita mwanafunzi mmoja mmoja.
Walimu wa shule ya msingi Nyololo hawakutaka kuzungumzia tukio hilo kwa madai kuwa hawafahamu undani wake, wakati taarifa za awali zilisema baada ya wanafunzi hao 18 kulalamikia ukatili huo kwa wazazi wao, viliitishwa vikao vilivyowajumuisha wakazi wa Nyololo, wazazi/ walezi, walimu, viongozi wa shule nawa serikali ya kijiji cha Nyololo.
Kwa upande wa wazazi na walezi wa wanafunzi waliofanyiwa ukatili huo, walisema katika kikao cha kumuhoji mwalimu huyo, alikiri kutekereza ukatili huo na kuomba msamaha kwa madai kuwa anashida za kimila na kuwa tukio hilo limewakosesha majibu.
“Yaani hata ninakosa majibu, nini kimesababisha mwalimu huyo afanye hicho alichowafanyia watoto wetu, alikuwa anachukua nini kwenye nyeti za watoto wetu?? Alikuwa anatafuta nini kwa mtoto wa miaka kumi na moja jamani” Alisikika Beatrice Petro mzazi mmoja wa wanafunzi waliofanyiwa ukatili akilalamika kwa uchungu.
Zoezi linahamia katika hatua nyingine ya kuitafuta kamati ya shule ya msingi Nyololo, na nikafanikiwa kumpata Richard Utulo - ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Nyololo, na anakiri kulifahamu tukio hili.
“Ni kweli tukio hilo limefanyika, na baada ya kupata taarifa hizo tulitisha kikao ili kuwahoji wanafunzi ambao walieleza kila mmoja alichofanyiwa, na pia tukamuhoji mwalimu kwa kumbana akakiri kufanya tukio hilo, zilifanyika taratibu mbalimbali ikiwemo la kumfikisha kitui cha polisi”. Alieleza Richard Utulo- Mw/kiti wa Kamati ya shule ya msingi Nyololo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi, alipopigiwa simu alisema hana taarifa ya tukio hilo, na kuwa atanipigia simu baadaye.
“Sina taarifa ya tukio hilo nitakupigia baadaye” Alisema ACP Bukumbi.
0 Comments