Header Ads Widget

WAJUMBE WA EALGA WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA SERA YA UGATUAJI MADARAKA

 



Arusha



Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,David Silinde amesema serikali ya Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika ugatuaji wa madaraka kwa kuanzia ngazi za serikari za mitaa na kuweza kuwafikia wananchi husika.



Akizungumza baada ya kufungua mkutano wa jumuiya ya Afrika wa serikali za mitaa(EALGA)uliowakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama wa EAC,Silinde amesema ugatuaji wa madaraka umesaidia kuwashirikisha wananchi moja kwa moja katika masuala ya utelezaji wa mambo mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.



Naibu waziri huyo amesema wananchi katika nchi ya Tanzania wamekuwa wakishiriki kuibua miradi ya maendeleo na serikali hubaki kutekeleza kwani hapo awali maamuzi yote yalikuwa yanatoka serikalini.



vilevile alisema katika michakato ya kibajeti kwa upande wa  ugatuaji wa madaraka michakato lazimia ianzie chini lakini hapo awali maamuzi yalifanyikia juu,jambo kubwa ni kuhakikisha kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa wanahitaji waharakishe kuweza kufikiwa na utekelezaji wa sera hiyo.



"Lengo la mkutano huu ni kuendelea kujadili dhima kuu ya ugatuaji wa madaraka katika kurudisha chini kwa wananchi hivyo tunapokutana hapa kwa nchi hizi wanachama ni kupena nafasi  ya kubadilishana uzoefu namna ya kutekeleza sera hii,"alisema Silinde.



Silinde alisema kubadilisha uzoefu wa sera wa ugatuaji wa madaraka kutawasaidia kuwapa nafasi ya kujifunza namna nchi nyingine zinavyotekeleza sera hiyo.



Aidha alisema kuwa ajenda nyingine ni kuhakikisha muungano huo wa jumuiya ya Afrika mashariki ili kuweza kuwa wamoja katika kutekeleza makubaliano ya awali pindi EAC inaanzishwa kwani yapo yaliyokamilika na mengine bado yapo kwenye utaratibu.



Awali akiongea katika Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Christophe Bazivamo amesema kwamba ipo haja kuishirikisha jamii nzima ya wanajumuiya hiyo kuweza kuona jamii ya wanaafrika mashariki

wakiongeza wigo wa kushiriki katika maandalizi ya bajeti zetu kutoa maoni yao.



Amesema serikali zetu kwa kushirikiana na jumuiya hiyo zimekusudia kuungana na kuchagua kupitia kifungu cha saba kwa

kushirikiana jamii na sekta binafsi katika kukuza maendeleo ya Pamoja kwa washika dau wote.



Ameongeza serikali za mitaa ndio ufunguo wa kuifikia jamii nzima

kuweza kushiriki kwa Pamoja katika kuuandaa sheria na bajeti zitakazosaidia kuwezesha jamii kuweza kupiga hatua za kimaendeleo ndani ya wananchi wa jumiya ya Afrika mashariki.



“Huu ndio msingi mkubwa wa kuwa na jamii inayoshirikishwa tumeona Tanzania imefanikiwa sana katika Ugatuzi wa madaraka hivyo tupo Pamoja katika kufikia malengo ya jumiya kuweza kusaidia serikali za nchi wanachama kufikia kuwezesha na kuibua miradi ya maendeleo kuanzia ngazi za chini,"amesema Silinde



Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,John Pima ameeleza kwamba mambo

yatakayojadili ni suala la ugatuzi wa madaraka ambao jiji la Arusha linautekeleza kwa kuwepo na uchaguzi wa kidemokrasia kuanzia ngazi za

chini Pamoja utawala bora.





Pima amesema shirikisho hilo lilianzia mkoani Arusha miaka ya 2002 hivyo sasa unaona jiji letu kwa mfano shule zetu zina Bodi za shule


hizi ni ugatuzi wa madaraka zamani utaona vitu kama hivyo vya shule vinasimamiwa na wizara ila sasa ni wananchi wenye ndio wanasimamia uendeshaji.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI