Mkuu wa mkoa wa Arusha john Mongella
Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amewataka viongozi wa halmashauri na wataalamu wake kushirikishirikiana na jamii katika kuwafichua waharifu ambao watakaohujumu miundombinu ya anuani za makazi.Mwandishi Teddy Kilanga MDTV Arusha
Akizungumza februari 12,2022 wakati wa kuzindua mfumo wa zoezi la anuani za makazi sambamba na kugawa miongozo,Mongella amesema haiwezekani serikali iweke miundombinu hiyo alafu wanatokea baadhi ya watu wanaihujumu kwa kuiondoa mahali ilipowekwa
"Watu wengine wanatoa chuma za anuani za makazi na kwenda kuziuza hivyo ni vyema wakuu wa wilaya na viongozi wa halmashauri mkashirikiana na jamii kuwakamata ili wachukuliwe hatua na kuwa funzo kwa wengine,"alisema.
Aidha Mongella amesema zoezi hilo la anuani za makazi zinamuhusu kila mmoja kuanzia mwananchi pamoja na viongozi wa mkoa hivyo ni vyema likasimamiwa ipasavyo katika utekelezaji wake.
"Napenda kuliweka sawa jambo hili kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi zoezi la anuani za makazi liwe shirikishi katika kuwahusisha viongozi wote wa ngazi zote kwa kufanya hivyo laweza kukamilika hata mwezi aprili 2022,"amesema Mongella.
Mongella amesema ushirikiano na ushirikishwaji ndio utakaopelekea zoezi hilo kukamilika haraka na halmashauri zitumie utaalamu wake katika kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kutengeneza vitendea kazi zitakazosaidia kukamilisha kwa mfanisi.
Mkuu huyo amesema Desemba,2021 baadhi ya wataalamu wa halmashauri nchini walipewa mafunzo kwa ajili ya zoezi la anuani za makazi ili wawaelimishe wengine hivyo ni vyema wakuu wa wilaya wakurugenzi na viongozi wote wa mkoa wa Arusha wakatekeleza wajibu wao katika kuhamasisha wananchi.
Vilivile amesema suala la anuani za makazi ni nyenzo muhimu kwenye maendeleo katika jamii na zoezi hilo likikamilika litabainisha makazi mbalimbali ya watu na wamiliki pia wa maeneo hali ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya ardhi.
Naye Mkurugenzi wa jiji la Arusha,John Pima amesema kwa upande wa halmashauri ya jiji la Arusha walianza zoezi hilo tangu mwaka 2008 ambapo zilifanyika kwenye kata nane ikiwa nne ndizo zilizokamilika na sasa wanaendelea kuzikamilisha.
"Niwaombe wananchi wa jiji la Arusha pamoja na viongozi mbalimbali kushirikiana katika zoezi hili ikiwa maana ya alama hizi ni kwamba hatutakwenda posta badala yake tunaletewa barua nyumbani pia zitaondoa gharama za kufungua sanduku la posta,"amesema.
0 Comments