Header Ads Widget

SIMBA SC MOTO MKALI CAF

 


Mchezaji Papa Sakho alivyowainua mashabiki wa Simba dakika ya 12 akifunga bao kwa  Acrobatic akipokea pasi ya Shomari Kapombe hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu mnamo dakika ya 60 Stephane Aziz Ki aliisawazishia timu yake ya Asec Mimosas baada ya kusawazisha wenyeji walianza kulishambulia lango la wageni kama nyuki.

Dakika ya 79 Simba walipata penalti iliyofungwa na Shomari Kapombe baada ya mlinda mlango Abdoul Cisse kumchezesha madhambi Yussuph Mhilu ndani ya 18.

Simba waliendelea kuliandama lango la Asec winga hatari kutoka Malawi Peter Banda alipigilia msumari wa tatu  dakika ya 81 akimalizia mpira wa John Bocco.

Kwa ushindi huo Simba wanaongoza Kundi D kwa  Pointi tatu na mchezo mwingine wa kundi hilo RSB Berkane watakuwa nyumbani majira ya saa nne kucheza na US Gendarmerie.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI