Header Ads Widget

SHIRIKA LA HAKIMAMA KUOTESHA MITI 20000 KUZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO



NA WILLIUM PAUL, Moshi.

 

KATIKA kuhakikisha Taifa linapambana na mabadiliko ya tabia ya nchi shirika la utunzaji wa mazingira lisilo la kiserikali la Hakimama linategemea kuotesha miti zaidi ya 20000 kuzunguka mlima Kilimanjaro.

 


Hayo yamebainishwa na msemaji wa shirika hilo Nderingio Mringo katika mkutano uliowahusisha Wenyeviti wa mazingira kutoka katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ya mlima Kilimanjaro ambapo alisema kuwa shirika hilo limekuwa likipambana kuhakikisha linatunza mazingira.

 


Mringo alisema kuwa, mazingira ya m ima Kilimanjaro yanaendelea kuathiriwa hali anbayo imekuwa ikichangia mabadiliko mbalimbali ya mazingira na hali ya hewa pamoja na ukosefu wa mvua na maji na ongezeko la joto na ukame.

 

“Uharibufu wa mazingira kwa kiasi kikubwa umepelekea kupoteza rasilimali mbalimbali za msitu, upungufu wa tija ya mazao ongezeko la umaskini hali ambayo imelekea kuanzisha shirika hili la Hakimama ili kutatua tatizo la uharibifu wa mazingira na msitu wa mlima Kilimanjaro” alisema Mringo.

 


Msemaji huyo wa shirika alisema kuwa, ili kutatua tatizo la mabadiliko ya mazingira yam lima Kilimanjaro kunahaja ya kuungana vijiji vyote katika shughuli za kulinda, kutunza na kutumia mazingira, rasilimali za asili na msitu kwa chini ya mfumo wa mmoja na sera ya mmoja.

 


Alisema kuwa, mwaka jana shirika hilo lilifanikiwa kuotesa miti zaidi ya 2000 huku kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wanatarahia kuotesha miti 20200 katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ikiwamo eneo la hifadhi ya mlima huo.

 


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirika hilo, Joseph Malya alisema kuwa, shirika hilo lilianzishwa mwaka 2019 ambapo lilimpata mfadhili kutoka nchini Japan  ambapo kwa sasa wanavitalu vya miche ya miti katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.

 


Malya alisema kuwa, miche hiyo ambayo wamekuwa wakiizalisha wamekuwa wakiotesha katika maeneo mbalimbali ili kupambana na ukame na kuurudisha mkoa wa Kilimanjaro katika hali yake ya awali ya kuwa kijani kibichi.

 

Mwisho…….

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI