Header Ads Widget

RAIS SAMIA AWAPA MAAGIZO WAKUU WA MIKOA.

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa Mikoa kuhakikisha hadi kufikia Mei 2022 mfumo wa zoezi la anwani za makazi uwe umekamilika.


Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wakuu wa Mikoa kuhusu mfumo wa Anwani za makazi ambapo mradi huo umeghalimu jumla ya shilingi Bilioni 28 kutoka bilion 700 huku Rais samia akisema fedha hizo zinakwenda kugawanywa kwa mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar. 


"Sitarajii kuona mkuu wa mkoa yoyote atashindwa kukamilisha zoezi hilo pale ifikapo mwezi huo," amesema Rais Samia


Aidha amewataka wakuu hao kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kama Uperesheni katika muda ulipangwa kwa kuwashirisha wananchi kama ilivyokuwa kwenye ujenzi wa madarasa ya UVIKO 19 ili kuweza kukamilisha zoezi zima la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kifanyika mwezi Agasti mwaka huu


"Itakapofika mei Mkuu wa Mkoa hakumali zoezi halifanyika vizuri tutakaa ana kwa ana tuelezane Kama unapata changamoto wakati unatekeleza sema haraka tukusaidi tukusaidie ziondoke uendelee na zoezi lakini utakapo kaa na changamoto zako na ukashindwa kumaliza tutakaa ana kwa ana tuelezane," amesema Rais Samia Suluhu Hassan 


Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amesema maendeleo ni watu na mfumu huo ni nyenzo ya maendeleo ya watu kwa kupitia mfumo huu watu wanawasiliana na mfumu huu ni mfumo wa utawala nani nyenzo  muhimu ya utawala. 


"Niwaombe kila moja wetu aliomo humu ndani twende tukawaelekeze wenzetu kuhakikisha wanatumia mfumo huu wa anwani za makazi ,"amesema Dkt Mpango. 


Naye Waziri wa habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Rais Samia ameamua kuijengaTanzania ya kidigitali kwani  mfumo wa anuani ya makazi ni moja ya hatua muhimu ya kuijenga tanzania ya Kidigital.


Mfumo wa anuani za makazi unatija kwa nchi na wananchi wake katika dhama hizi za digital kwani unamtambulisha mtu alipo anapopatikana au kuhudumiwa iwe nyumbani ofisi au sehemu ya biashara .


Mfumo huo utawezesha uchumi wa kidigital nchini hivyo ni muhimu kutambua Maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanategemea sana mifumo ya kitambuzi hususani mfumo wa anuani ya makazi. 


Mw

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI