Header Ads Widget

MISITU UCHANGIA ASILIMIA 3.5 YA PATO LA TAIFA

 




WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro amesema Misitu inachangia 3.5 ya Pato la Taifa huku akisema Wizara  yake kupitia Taasisi ya huduma za MisituTanzania (TFS) wamejipanga kuifanya Tanzania kuwa ya kijani ........Na Hamida Ramadhan Dodoma 


Amesema Tanzania itakuwa ya kijana endapo tu mamabo mawili yatafanyika ikiwa ni pamoja na kulinda misitu tuliyonayo isivamiwe isiharibiwe na  isikatwe hovyo tunaruhusu matumizi endelevu ya misitu nasio matumizi ya hovyo ya misitu.


Hayo ameyasema leo jijini hapa wakati alipouwa akiongea na waandishi wa habari kwenye zoezi la upandaji miti linaloendelea katika wiki ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 12 jijini Dodoma. 


" Tuendelee kupanda miti kwasababu hata tusipo kata kuna miti inakuwa na inazeeka inakufa lazima tupande miti mingine tukikata miti ni lazima tupande miti  ili Tanzania iwezekuwa ya kijani tukumbuke misitu ni mali kwasababu kunawatu wanaishi kutokana na misitu watu wanauza mbao Maginga na Iringa. 


Amesema Misitu inachangia pato la Taifa kwa asilima 3.5 inazidi sekta nyingine ambazo watu hawazijui ndio maana tunasema misitu ni mali watu wanafanya biashara ya mbao,biashara Samani bila kusahau misitu ndio chanzo cha mazingira mazuri tuliokuwa nayo.



Kwa upande wake Profesa Dos Santos Silayo kamishina wa Uhifadhi Tanzania (TFS) wanashiriki katika juma hilo ambapo amesema Mazingira ni dhana pana  na inamasuala mabalimbali yaliomo ndani yake ila sehemu kubwa ya mazingira ni Misitu .


Amesema tuanapoongelea misitu tunagusa sekta ndogo ya nyuki ili kufikia malengo hayo na ndio maana tuko hapa  tukifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupanda miti.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk.Andrew Komba amesema  kuwa wameweka alama Iyumbu kwa kupanda miti na kwamba katika wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira walipanda miti hiyo.


Ameongeza kuwa katika tukio hilo walilolifanya la kupanda miti  lilianza tangu Februari 7 na  linatarajiwa kuhitimishwa Februari 12,mwaka huu ambapo wamefanya shughuli mbalimbali za  kupanda miti katika eneo la Medali na  kufanya usafi katika maeneo ya barabara ya Ilazo inatokea Wajenzi.


"Sehemu hii ya Iyumbu wenzetu wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wametenga eneo hili kama eneo la hifadhi linapaswa kupandwa miti wenyewe wanasema ni eneo la kijani (Green Park),eneo la kijani,"amesema.


Mkurungenzi huyo amesema kesho watakuwa soko la Chang'ombe kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kusimamia taka na kuzitenganiasha kwa kwa sasa taka hizo ni mali.


Ameeleza kuwa wataoa elimu ya kutenganisha taka ngumu na zile za vyakula na kwamba taka hizo zinaweza kutenganezwa kuwa mkaa kwa baadhi yao.


Katika zoezi hilo la upandaji miti na kutanya usafi wameshirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wananchi na wanahabari.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI