Kampuni ya Jatu (PLC) imeiyomba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwashika mkono/kuwasapoti juu ya kazi wanazozifanya ambazo zimekua zikitoa matokeo chanya ikiwemo kutoa ajira rasmi 500.,........Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Jatu PLC, Mohamed Simbano wakati walipokua wakitiliana saini Balozi wao Mrisho Mpoto kwa mara nyengine tena ambapo wamempa ubalozi wa miaka 3 kuendelea kuitangaza kampuni hiyo katika mikoa mbalimbali.
Amesema kuwa, licha ya kumpa ubalozi huo lakini pia wamemuandalia kipindi maalum cha (Kaa Hapa) kitakachorushwa na kituo cha chanel 10, ambapo kampuni hiyo imekua ikiunga mkono juhudi mbalimbali inazofanywa na Rais Samia, katika kuleta maendeleo kwa wananchi ambapo wamekua wakifanya shughuli mbalimbali zinazolenga kuinua uchumi kwa wananchi.
"Lengo la kipindi cha "Kaa Hapa" hapa awamu ya pili ni kuitangaza miradi mbalimbali ikiwemo Kilimo, Ufugaji, Maji, ujenzi na utalii inayofanywa chini ya uongozi wa Rais Samia, kwetu sisi Sekta ya maji ni nguzo muhimu katika kuleta mapinduzi ya kilimo, hasa cha umwagiliaji ambacho tumekua tukifanya mikoa mbalimbali"amesema Simabo.
Hata hivyo, amesema wameweza kufanya mambo makubwa kwa kipindi cha miaka 5 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo, ikiwemo kuingiza kampuni ya Jatu Plc katika Soko la hisa la DSE, kufungua ofisi kikanda ndani ya nchi na Afrika Mashariki kwa kuanza na Kenya kwa lengo la kupanua wigo wa masoko ya ndani na nje.
Sambamba na hayo pia wameweza kufungua bima ya kilimo na Ufugaji, kuwepo kwa ongezeko la wakulima zaidi ya elfu tano, kutoa ajira rasmi 500 na zisizo rasmi zaidi ya 10000, kuchochea maendeleo kwa kulipa kodi mbalimbali pamoja na kukuza kipato cha wakulima kwa kuweka mifumo wezeshi na kufanya uwekezaji wa pamoja kupitia kampuni ya umma ya Jatu PLC.
Hata hivyo, amesema asilimia 95 ya kampuni hiyo inamilikiwa na watanzania wa kawaida kabisa ambao wengi wao ni vijana, kina mama, makundi maalum, wazee pamoja na watumishi kutoka Sekta tofauti tofauti.
Kwa upande wake, Balozi wa Kampuni hiyo, Mrisho Mpoto ameishukuru sana kampuni hiyo kwa kumuamini kwa kumpa tena ubalozi wa miaka 3, kwa lengo la kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwemo hisa, viwanda, masoko, kilimo na Ufugaji ambapo mambo yote hayo na mengine mengine utayasikia kupitia kipindi maalum kitakaruka kupitia Chanel 10.
Aidha, ameiahidi kuitendea mambo makubwa kampuni hiyo katika kuitangaza juu ya kazi wanazozifanya na kuwataka wadau mbalimbali kujiunga na kampuni hiyo ili kuweza kulima kisasa na kampuni ya Jatu PLC.
"Juzi tarehe Saba niliteuliwa kuwa Balozi wa maji nchi nzima, na Leo tarehe Tisa nimechaguliwa tena kwa awamu ya pili kuwa Balozi wa Jatu, ni jambo la kumshukuru Allah kwa madili haya yanayofungunguka kwangu, niwaombe wadau waendelee kuja iunisapoti tufanye kazi "amesema Mpoto.
0 Comments