Madaraja mengine mawili yamepatikana ili kujengwa katika mto Mzinga huko katika kata ya Tambani Wilaya Mkuranga mkoani Pwani kwa lengo la kumaliza kero kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga na sehemu ya jiji la Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga Mheshimiwa Abdallah Ulega wakati akizindua daraja la Tambani katika mto huo Mzinga.
Amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa CCM taifa kwa kushirikiana na uongozi wa Mbagala jijini Dar es salaam amepata matumaini ya kupata tena madaraja mengine mawili kwa ajili ya wananchi wanaovuka mto Mzinga.
0 Comments