Header Ads Widget

KAULI YA NAPE ICHUKULIWE KWA TAHADHARI - ACT

 



Na MWANDISHI WETU


Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa tahadhari tamko la Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kuyafungua magazeti  kadhaa ambayo yalikuwa yamefungiwa  na pia kuahidi kupitiwa kwa sheria kandamizi ya vyombo vya habari iliyopitishwa mwaka 2016 na kuzuia ukuaji na upanukaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini.


Msemaji Kivuli wa ACT Wazalendo kwenye eneo la habari, Ally  Saleh (Alberto) amesema leo Februari 10, 2022 Mjini Unguja Zanzibar ambapo amesema taifa linawajibu kusubiri na kuona udhati wa Serikali katika kilichosemwa na Waziri Nnauye, na kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kuona kuwa sekta hii inaweza kuwekeza nchi za nje bila ya kutandikwa misingi makini.


Alisema kuna kazi kubwa ya kufanya kabla ya kuota ndoto ya kuwa na mashirika ya kimataifa ambapo mbali ya changamoto za kisheria na za kisera zilizojaa kithiri pia kuna changamoto za kikodi ambazo wawekezaji kwenye sekta hii wanakabiliana nazo.


Pia Saleh alisema, “ Imechukua mwaka mzima kwa  Serikali kufungulia magazeti yaliokuwa yamefungiwa  yaliotajwa kuwa ni pamoja na MWANA HALISI, TANZANIA DAIMA, MAWIO na MSETO ambapo Serikali hiyo hiyo inajificha katika kivuli cha kuwa magazeti hayo yalifungiwa katika wakati wa utawala kandamizi wa Rais aliyepita John Pombe Magufuli,” alisema Saleh.


Magazeti haya yanafunguliwa bila ya Waziri Nnauye kuelezea iwapo kuna mpango wowote wa kuyasimamisha upya. Inawezekana amri ya kuyafungulia isiwe na maana kwa sababu pengine hayatakuwa na uwezo wa kifedha kurudi mtaani, alitahadharisha Saleh.


Saleh alikubali kuwa ni kweli palipita kipindi kigumu lakini ni muhimu kama taifa kujenga misingi ili hali kama hiyo ya kuzuka utawala wa kidekteta isijirudie. “ Tunapaswa kama taifa kujenga misingi imara ya kidemokrasia ili utawala wa nchi usitegemee utashi wa mtu. Misingi hiyo izame kwenye katiba na sheria zetu.”


Saleh alieleza kuwa misingi mkuu wa kuipitia sheria mbovu za habari ziliopo nchini ni kuwashirikisha wadau halisi wa vyombo vya habari. “ Tunakubali nia hiyo ya Serikali lakini ushirikishwaji uwe wa nia na dhati ili kujenga taifa lenye uhuru wa habari. Serikali sio mdau peke yake wa habari na ikumbukwe kuna umma mzima upande wa pili.”


Dhana kuwa waandishi wa habari ni wadau wa maendeleo, isiwe upande wa kuwatumia waandishi wa habari tu kwa kuwarembaremba, lakini ni kuheshimu mawazo yao, hata yale yanayotofuatiana, Saleh alisema na kutaka mahusiano ya wana habari na Serikali yawe yaliotandikwa katika msingi wa pande zinazojitajiana.


ACT Wazalendo alisema Saleh inatoa wito kwa Waziri Nnauye na Serikali sio tu kupitia sheria ya Magaeti ya 2016 lakini pia kuna sheria nyingi zenye mnasaba na kujenga uhuru, ustawi na uendelezaji wa vyombo vya habari ambazo zinapaswa zitizamwe na zirekebishwe katika kipindi kinachopimika.


“Kwa ufupi sekta hii nzima imejaa miiba na mbigili…Tunapaswa kuondosha miiba na mbigili zote kama tuna nia ya kutaka kupimwa tufanane na hadhi ya kilimwengu katika suala la uhuru wa kutoa, kupokea na kusambaza habari,” Saleh ambaye ametumikia fani ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miongo miwili amesema.


Alizitaja sheria hizo ni kama vile Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sheria ya Usalama wa Taifa, Sheria ya Bunge, Sheria ya Haki ya Kupata taarifa, Sheria ya Makosa ya mtandao, Sheria ya maudhui ya utangazaji na nyenginezo kwenye sekta hii.


ACT Wazalendo, alisema Saleh,  iko tayari kutoa ushirikiano na mawazo katika kuiimarisha sekta hii ya habari na teknolojia ya habari na kuongeza kuwa, “Kwa kuwa sote tunajenga nyumba moja, niko tayari kukutana na Waziri Nnauye tuone kwa pamoja tunawezaje kurejesha heshima ya fani hii kwa kuchanga mawazo yetu na 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI