Header Ads Widget

KATA YA LEVOLOSI LAHITIMISHA ZOEZI LA UTAMBUZI WA ANWANI ZA MAKAZI KUFUATIWA NA CODE NET

 


Arusha


Kata ya Levolosi iliyopo halmashauri ya jiji la Arusha imefanikiwa kukamilisha zoezi la utambuzi wa anwani za makazi ili kuingia kwenye hatua ya uwekaji wa majira ya nukta(Code net)


Akizungumza februari 17,2022 baada ya kuhitimisha zoezi hilo lilodumu wa ndani ya siku tatu,Mratibu wa kata ya Levolosi,Haliye Abubakar alisema wamefikia nyumba takribani 540 na mitaa ipatayo 32.


"Zoezi limechukua muda mfupi kutokana na ushirikiano mzuri na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa mitaa hii tuliyoipitia japo tulipata changamoto siku ya kwanza tukawaelimisha na wakaelewa hivyo siku zilizofuata tulifanya kazi kwa urahisi sana,"alisema Abubakar Mratibu wa zoezi hilo,"alisema.


Aidha Abubakar alisema zoezi linaloendelea februari 18,2022 ni uwekaji wa majira ya nukta katika nyumba na barabara zote zilizofanyiwa utambuzi wa anwani za makazi.


Nao baadhi ya wananchi walioshuhudia zoezi hilo likiendelea katika baadhi ya kata zilizopo jijini Arusha walisema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa  kuleta zoezi hilo kwani walikuwa wanapata tabu katika kuwaelekeza wageni na kugharamikia fedha nyingi.



Emmanuel Kessy ni mmoja wa wananchi hao ambapo alisema hayo ndio maendeleo yaliyongojewa na wananchi kwa muda mrefu,Tanzania kuwa ya kimataifa kwani katika nchi zilizoendelea zoezi la anwani za makazi lipo muda mrefu na linasaidia kuokoa muda.


"Zoezi hili likikamilika litatusaidia katika kuleta maendeleo kwa wakati ikiwa serikali itafahamu idadi ya makazi kupitia anwani hizo,pia itatusaidia sisi kama wananchi kuachana na mambo ya posta ambayo yalikuwa yanatupotezea muda na kuongeza gharama,"alisema Kessy.



Zoezi la utambuzi la anwani za  makazi limekamilika katika kata tano ikiwemo,Levolosi,Kaloleni,Themi,Sekei na Kati ambapo februari 18,2022 wanaendelea na uwekaji wa majira nukta.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI