Header Ads Widget

DIWANI LYDIA MGAYA AMTUMIA RAIS SAMIA SALAMU ZA VALENTINE

 


Diwani viti maalumu jimbo la Kibaha mjini Mheshimiwa Lydia Mgaya amemtumia salamu za Valentine Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwataka watanzania wote kumpongeza kwa dhati na kumuunga mkono katika utendaji wake wa kazi za kuongoza nchi.


Ametuma salamu hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari huko mjini Kibaha.


Amesema yeye ameona aelekeze salamu zake kwa Mheshimiwa Rais Samia kwani ni Rais anayewapenda watanzania wote "Ni Rais mwenye moyo wa upendo kwa Watanzania wote na anajali kila mmoja habagui masikini wala tajiri wakubwa kwa wadogo tumeona kwa macho yetu"


"Tumeona Rais Samia anapambana kwa ajili yetu watanzania na hasa ukizingatia ni Rais wa kwanza mwanamke mwenye juhudi ya maono kwa taifa letu kama yeye katika Afrika mashariki yote"

 

Lydia amesema kinachomfurahisha zaidi kwa Rais Samia ni tabia yake ya kujiamini ambayo alioonesha tangu anaingia madarakani.


Amesema Watanzania tuonyeshe pia na sisi tunapenda kwa juhudi anazofanya katika nchi yetu.


Akizungumzia ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari nchi nzima Lydia amesema "tulikuwa tunaona jinsi Wanafunzi walikuwa wakibanana madarasani lakini yeye ametukomboa kwa kujenga madarasa 15000 ambapo sasa hakuna kero hiyo tena wala hakuna anayekosa vipindi kwasababu ya ukosefu wa madarasa.


Amesema madarasa hayo yamejengwa vizuri na kwa kasi ya ajabu ambapo kwa muda wa mwezi mmoja madarasa yamekamilika.


Kwa upande wa kuwawezesha Kundi la Wasanii nchini amesema fedha tayari zimeingizwa kwenye akaunti ya wasanii sambamba na mikopo ya halmashauri kwaajili ya kundi la Kinamama, vijana na walemavu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI