Teddy Kilanga_ Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda ameipongeza halmashauri ya jiji la Arusha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mfumo wa zoezi la anwani za makazi ili kuondoa malalamiko miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa wenyeviti na watendaji wa mtaa yenye lengo la utekelezaji wa kazi ya anwani za makazi jijini humo,Mtanda alisema kuwashirikisha wadau katika zoezi hilo ni jambo jema ili kuepuka upotoshaji unaoweza kujitokeza kwa watu wasiopenda maendeleo.
"Kwa hiyo mmefanya vizuri kuwahusisha wadau waelewe umuhimu wa zoezi la makazi maana yake nini,lakini ni vyema mkafanya kazi kwa umoja na mshikamano ili iweze kukamilika kwa wakati hadi kufikia machi mwaka huu liwe limekamilika,"alisema Mtanda.
Mtanda alisema ni vyema wenyeviti wakafuata yale waliyoelekezwa kupitia mafunzo hayo na kuacha kuanzisha utaratibu wao wenyewe ambao unaweza kuleta mitafaruko katika jamii hali ambayo inaweza isifikishe muhafaka wa zoezi hilo.
Pia alimtaka Mkurugenzi wa halmashuri ya jiji hilo ,Dkt.John Pima kuhakikisha haki wasimamizi wa zoezi ho zinalipwa kwa wakati ili waweze kufanya kazi vizuri kwani haki inaenda sambamba na wajibu.
"Tunataka nyinyi watendaji na watumishi wa serikali muwe kiunganishi kizuri baina ya serikali na wananchi kwani mkitekeleza vizuri kazi zenu wananchi wataipenda serikali hii na tutakuwa tunafaidika sote,"alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,Dkt.John pima alisema zoezi hilo limezindulia rasmi na Mkuu wa wilaya huyo Said Mtanda ikiwa kimkoa walizindua mnamo februari 22,2022 na Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella.
Dkt.Pima alisema zipo baadhi ya kazi zimeshafanyika kwa lengo la kuandaa timu pamoja na zoezi la utoaji wa elimu ambapo watendaji na wenyeviti wa mtaa ndio watakaokwenda kuhitisha vikao vya kwanza katika utambuzi wa barabara kwenye maeneo yao.
"Timu hii ndio ambayo inatakiwa iandike muhitasari na izingatie utaratibu wa kuleta majina hayo na namna ambazo nyumba zitapangwa kwani ndio inayohusika na kufahamu maeneo yote,"alisema Dkt.Pima.
Mkurugenzi huyo alisema kata ambazo wataanza nazo ni kaloleni,kati,Levolosi,Themi, pamoja na sekei ifikapo februari 28 mwaka huu ziwe zimekamilika kwani hatua walizochukua hadi sasa ni kuandaa watendakazi ikiwa baadhi yao watatoka miongoni mwa watumishi wa halmashauri hiyo.
Aidha alisema kata hizo zitaanza Februari 14,2022 ikiwa taratibu zote zimeshakamilika na kata 20 zilizobaki litaanza februari 21,2022 kutokana mchakato wa kutafuta watumishi wa muda wa zoezi hilo.
0 Comments