Na Rehema Abraham , Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Moshi vijijini Cirily Mushi amesema kuwa Chama kipo tayari kuwatetea wale wote wanaoonewa na kuwata wote wote wanaoona wanaoonewa kuripoti kwa viongozi wa Chama hicho ili waweze kusaidiwa.
Mwenyekiti huyo amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 45 ya kata ya mabogini yaliyofanyika mabogini mkoani Kilimanjaro.
Aidha amesema kuwa ni jukumu la viongozi wa Chama hicho kuhakikisha kuwa wananchi wa mabogini wanatatuliwa kero zinazowakabili.
"Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba kero mbalimbali haziendelei kukera wananchi wetu na kuwakosesha Imani ,lakini pia hatuwezi kuwa na nchi ya wanyanganyi ,wadaanganyifu na walaghai "Alisema Mushi.
Amesema kuwa Kuna mambo mengi yamebadilika tangu kuanzishwa kwa Chama Cha mapinduzi na kusema kuwa bila kuyaasema hayo hawatendi haki kwa viongozi waliotangulia.
Hata hivyo Amesema maendeleo yaliyofanyika na Serikali yamefanywa na Chama Cha mapinduzi kwani huwezi kutaja maendeleo bila kutaja Chama Cha mapinduzi CCM.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Moshi Ramadhani Mahayu amewataka viongozi wa kata hiyo akiwemo mbunge wa Jimbo na diwani wa kata kuhakikisha kuwa wanaitisha mikutano ya hadhara ili kusikiliza kero za wananchi na kuangalia ni namna gani wanaweza kuzitatua kero zinazowakabili.
Aidha amesema kuwa ni vyema mbunge anaporudi kutoka bugeni akatisha mkutano wa hadhara licha ya kwenda kutembea miradi ya maendeleo.
"Nimekuja kufanya kazi Moshi na lazima niafanye kazi vizuri na lazima pia niwashauri waheshimiwa viongozi wangu "Alisema
Hata hivyo diwani wa kata hiyo ya mabogini Bibiana Masawe amesema kuwa miradi iliyoelekezwa katika kata hiyo ni pamoja na miradi wa madarasa matatu shule ya msingi Benjamin Mkapa ambapo walipewa pesa milioni 60 Kutoka Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA )ambao umekamilika .
Sambamba na hayo mradi wa madarasa mawili ya Mabogini sekondari uliokuwa ukijengwa kwa nguvu za wananchi ambayo yalikuwa yamefikia zaidi ya milioni tisa , ambapo walipata pesa milioni 25 kutoka EP4R, milioni tatu kutoka mfuko wa Jimbo milioni 5 kutoka halmashauri.
Ameendelea kutaja miradi mingine ambayo yamejengwa kwa fedha za uviko 19 madarasa 7 , mabogini secondary na walipokea milioni 240, mradi wa madarasa 8 mpirani secondary walipewa milioni 160 .
Mradi mwingine ni mradi wa maji unaogharimu milioni 500 katika vijiji vya maendeleo, mtakuja na mserekia ambao unaendele katika vijiji ,na ujenzi wa barabara unaojegwa kutokana na kuwa kero kwa wananchi kwa Muda Mrefu.
0 Comments