Header Ads Widget

BENKI YA USHIRIKA MOSHI (KCBL)YASHEREKEA MWAKA MMOJA WA MAFANIKIO

 



Na Rehema Abraham, Kilimanjaro 


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Andrea Masawe  ameagiza benki ya ushirika Moshi (kcbl) kuendelea kutoa mikopo ,kwa wakulima ,vijana na wafanyabiashara  ndogondogo .



Ameyasema hayo wakati alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kusherekea  mwaka mmoja wa benki hiyo iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Aidha amemtaka pia benki hiyo kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu hasa kwa wakulima na wafanyabiashara wadogowadogo (machinga).


"Tumesikia na tumeambiwa kuwa benki zetu za bishara wakiwemo CRDB Sasa wameanza kutoa mikopo yenye riba ndogo na kwa mara ya kwanza tumesikia wameanza kutoa interest rate pasipo digit ,hii ni hatua muhimu kwa hiyo niwaombe benki kwa ujumla wake kuendelea kutoa riba ambayo ni single digits ili kuweza kusaidia sana kuendeleza sekta yetu ya kilimo" Alisema.


Katika hatua nyingine ametaka Tume ya maendeleo ya ushirika nchini ,chini ya mrajisi Mkuu kuendelea kusimamia benki hiyo ya ushirika .


"Wametokea kwenye Hali mbaya Kama tulivyoelezwa hapo awali kwa kupitia changamoto mbalimbali lakini tunaamini kwenda mbele Sasa ukasimamie kwa kufuata miongozo ,kanuni Sheria ,taratibu zinazotoa miongozo mbalimbali ya ushirika nchini"Alisema.


Hata hivyo amesema kuwa Wizara itahakikisha  kwamba inaboresha sera ya ushirika nchini na Sheria ya ushirika lakini amesema hilo  litafanikiwa kwa kushirikiana kwa ukaribu sana na benki kuu .


Kwa upande wake mrajisi wa vyama vya ushirika nchi Doct. Benson Ndiege amesema kuwa benki hiyo ya ushirika inakwenda kuwahudumia watu wote wanaotoka kwenye sekta mbalimbali , inakwenda kuwahudumia wafanyabiashara wadogo (machinga na mama ntilie).


"Nichukue fursa hii kuwataka kcbl kutokana na maelekezo ya mh. Rais juu ya kuwawezesha vijana na mamantilie ,chukueni nafasi hii kuhakikisha kwamba muelekeo huu wa Serikali kuchukua nafasi ya kuwafikia kwani hao ndio mrengo wa nchi"Alisema.


 Amesema kuwa time ya maendeleo ya ushirika Tanzania itahakikisha kuwa inasimamia benki hiyo ili iweze kufikia malengo walizojiwekea  .


Naye meneja wa benki hiyo Godfrey Ng'urah amesema kuwa moja ya mambo ya mfano ni pamoja na mgeuzi yaliyofanyika katika mfumo wa kiuendesheji ,usimamizi wa benki ,utoaji wa huduma ,pamoja na kuwa benki inayotoa huduma kwa makundi yate ya jamii hasa makundi maalum Kama vijana , wanawake.


"Lakini pia tumetanua huduma zetu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wakati na wafanyakazi wa sekta mbalimbali  kwa hivyo wigo umepanuka na kujitambua Kama benki ya jamii kwa ujumla wake na hii imetusaidia kufanya na kuongeza njia mbalimbali za kuongeza mapato ya benki ambapo kwa kipindi Cha mwaka mmoja timefanikiwa kuongeza mapato ya benki mpaka kufikia bilioni moja .


Hata hivyo mkurugenzi wa wa CRDB nchini Abdul Nsekela amesema kuwa anafurahi kuona kuwa benki hiyo ya ushirika kcbl imerudi katika Hali yake 


"Nafarijika kwamba bàada ya mwaka mmoja sisi kuingilia wamepata faida ya milioni 54 lakini wameelezea mikakati Yao ya kujipambanua kuwa benki ya kitaifa inayoangalia zaidi kilimo "Alisema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI