Header Ads Widget

AZAM TV WAPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE, WAFUNGUA DUKA ARUSHA

 




Teddy Kilanga_ARUSHA



Azam waanza kufungua ofisi ya kanda ya kaskazini ili kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kusaidia kutatua changamoto za visimbuzi.



Akizungumza  wakati wa uzinduzi duka la Azam TV  kanda ya kaskazini,Mkurugenzi mkuu wa Azam,Sabrina Muhamed Ally alisema uzinduzi huo umekuwa chachu katika kuwasogezea huduma wananchi ambao utawasaidia katika kutatua changamoto za wateja wao.



"Tangu Azam Tv ianze hii biashara 2013 tulikuwa tunaoperate kutoka Dar es Salaam ambapo waliwatumia mawakala waliokuwa wamesambazwa nchi nzima lakini kutokana na wateja kuhitaji huduma zilizokaribu zaidi hali iliyosababisha kufungua tawi hili kanda ya kaskazini,"alisema Mkurugenzi huyo.



Aidha alisema hawataishia katika kanda hiyo pekee bali watafungua katika kanda ya kati,ziwa pamoja na kanda ya kusini  hadi mwaka huu watakuwa wamemalizi kuzindua matawi katika kanda zote ikiwa dhamira yao ni kufikisha burudani kwa watu wote.




Naye Meneja mauzo wa AzamTv wa Tanzania,Adam Lyimo alisema lengo la uzinduzi huo ni kufikisha burudani kwa watu wote pamoja na kujongea karibu na mawakala wao,wadau pamoja na wateja kwa ujumla.



Alisema  huduma hizo zitakazotolewa ni pamoja na matengenezo ya visimbuzi bure kwa lengo la kustawisha jamii katika kuungana na serikali  kufikia uchumi  wa kati wa juu.



Naye mmoja wa wakazi wa Arusha,Abadi Mtengwe alisema  huduma kusogezwa karibu ni jamba jema kwani hapo awali waliwatumia mawakala lakini visimbuzi vinapoharibika walikuwa wanachajiwa gharama kubwa.


Sambamba na hilo alisema anamkumbuka mtangazaji Charles Hilary kupitia kipindi cha taarifa ya habari kwani alikuwa na baadhi ya vionjo vinavyowavutia watazamaji.



"Kweli nasikitishwa na Charles Hilary kuondoka Azam kwani alikuwa na mbwembwe sana katika utangazaji wake kutuwekea vionjo mbalimbali nitamkumkumbuka sana,"alisema Mwananchi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI