Header Ads Widget

"ASILIMIA 5 YA MAPATO YA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI HUPOTEA KWA UFISADI"_SHAKIBU




Na Hamida Ramadhan Dodoma



RIPOTI ya Kimataifa ya mwaka 2021 iliyotolewa na Taasisi ya taaluma ya kudhibiti Ufisadi Duniani (ACFC ) inasema asilimia 5 ya mapato yanapotea kwa ufisadi kwenye taasisi zote za Umma na binafsi.


Hayo yemesemwa leo jijini hapa na Shakibu Mussa Nsekela Bingwa katika masuala ya Ubadhilifu Kudhibiti Rushwa na Ufisadi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo taasisi za umma na binafsi kuweza kudhibiti ufisadi katika maeneo yao.


Amesema katika utendaji  utendaji kazi wao wamebaini kuwa ufisadi unaosikika ni ule unaosikika au kujulikana na ufisadi mwingi hazigunduliki au wahusika kuelewana wenywe kwa wenyewe na kupotea.


Amesema unapotokea ufisadi taasisi  hutumia gharama kubwa namna kwa kufanya uchunguzi ukaguzi na pesa zilizochukuliwa kuzirudisha inakuwa ni changamoto. 


"Tumeona njia bora ya kudhibiti ufisadi ni kuzuia ufisadi usitoke na inapotokea  tujenge taswira na  wahusika ipo siku watagundulika kuwepo na nia ya kuwatafuta watu kuwafatilia ili wagundulike," amesema


Na kuongeza kuwa" Kazi yetu kubwa tunawajengea uwezo taasisi za umma na binafsi juu ya dalili za ufisadi namna gani zinatokea na jinsi ya kuthibiti ufisadi ," amesema  Nsekela


Kwa upande wake Dkt Clement  Mashamba wakili wa kujitegemea  na Muhadhiri wa sheria mwandamizi amesema tatizo la ufisadi ni kubwa kwani watu wengi wanaamini kuwa ili uweze kuwa tajiri lazima ufanye ufisadi lakini pia zipo sababu za kusababisha tatizo hilo liwepo.


Amesema ufisadi unatokea kwa sababu kuna fursa za kufanya hivyo watu wanashinikizio na tatu kuwepo kwa  mianya na fursa watu kufanya ufisadi.


"Watu wamekuwa wakivunja sheria na taratibu zilizowekwa lakini usimamizi ni mdogo hali inayopelekea ufisadi kuendelea kutokea kikubwa tuangalie upya sheria zetu ili ziweze kubana mianya ya ufisadi na mambo yanayoibuka mapya katika ufisadi kwani sasa ufisadi upo kwenye njia za kidigitali mitandao," amesema 


Naye Meshaki Shashi Kaimu mkuu wa idara ya uchunguzi wa ndani Benki ya Taifa ya biashara  NBC amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yanawaweka pamoja ili nawao kwa umoja wao waende kupambambana na ufisadi katika maeneo ya taasisi za umma na binafsi.


" Ufisadi ni tatizo kuwa sio kwenye mabenki tu sehemu zote lakini kwenye benki yangu ya NBC ipo kama taasisi na ndio maana tupo hapa katika kuhakikisha kupeana uwezo kudhibiti uhalifu huu,"amesema 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI