Waziri wa Habari Nape Nnauye akiwajulia Hali wanahabari wanne wa Azam media waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ajali jana eneo la Kitonga Iringa wakati wakielekea Mbeya kurusha mechi za Ligi kuu ya NBC
WAFANYAKAZI 12 wa kampuni ya Azam Media wamejeruhiwa baada ya gari la kampuni lenye namba za usajili T735DHQ aina ya Toyota Hiace
waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya kugongwa na lori lililopata hitilafu katika mfumo wa breki na kurudi nyuma eneo la mlima Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa .
Ajali hiyo imetokea leo majira ya mchana na kupelekea barabara ya Iringa -Dar es Salaam kuzibwa Kwa masaa kadhaa kutokana na ajali hiyo ya Lori kuziba njia .
John Sanga mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo alisema gari la wafanyakazi wa Azam media lilikuwa nyuma ya Lori Hilo hivyo wakati Lori likirudi nyuma Kwa kushindwa kupanda mlima gari hilo la Azam lilishindwa kulikwepa Lori hivyo kugongwa vibaya .
Alisema iwapo dereva wa Hiace ya Azam angekuwa amechukua tahadhali Kwa kukaa mbali ya Lori kulikuwa na uwezekano wa kuepuka kugongwa na lori Hilo .
Hata hivyo alisema madhara makubwa hayakutokea kutokana na Hiace hiyo kuwa jirani na hivyo kutumia kama kizuizi cha Lori Hilo kuendelea kurudi nyuma
Kupitia kurasa ukurasa wao wa Instagram Azam Media wametoa taarifa iliyoeleza tukio Hilo la wafanyakazi wake kupata ajali kuwa walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya NBC na kwamba, wamesaidiwa na Jeshi la Polisi na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amelithibitisha Kwa njia ya simu alipozungumza na Matukio Daima Media kuwa hakuna kifo zaidi ya watu kama watatu hivi kujeruhiwa .
"Kwa Sasa bado nipo eneo la tukio likipambana kufungua njia ili magari yaweze kupita taarifa kamili nitatoa baadae ila hakuna kifo zaidi ya majeruhi"alisema Bukumbi
0 Comments