IKIWA imefika nusu mwaka ya Bajeti ya Serikali wadau wakupinga ukatili wa kijinsia wameiomba serikali mwaka wa fedha unaokuja kutenga Bajeti ya kutosha kwa ajili ya mpango mkakati wakupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili mapambano ya kumuokoa mwanamke na mtoto nchini dhidi ya ukatili yaendelee.
Akiongea jijini Dodoma Zainabu Mmari kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP ) Kama Afisa Program Mwandamizi Idara ya Utafiti na Uchambuzi amesema Serikali na Wizara zake zikitekeleza masuala ya MTAKUWWA kwa kutenga bajeti ya kutosha wanawake na Watoto wanaopitia vitendo vya kikatili watafikiwa na kukombolewa.
" Nisema hivi kwa sababu Serikali ni mdau mkubwa wa utekelezaji wa mpango huo wa MTAKUWWA nikweli tunafanya kazi kwa kuhakikisha tunamkomboa mwanamke na mtoto wa kike lakini wazi mpango huu hakuweza kutekekezeka vile tulivyotarajia kutokana na ufinyu wa Rasilimali fedha," amesema Mmari.
Aidha ameendelea kusema kuwa wao kama wanaharakati kupitia wadau wakimaendeleo huko mbele wanatamani kuona mwanamke anasimama mwenyewe kiuchumi kwani wanawake wengi wamekuwa wakipingwa kutokana hali duni ya kiuchumi ndani ya familia.
"Wanawake wengi wamekuwa wakipigwa kutokana na umasikini wa kipato katika familia mwanamke akiomba pesa kwa mumewe amekuwa wakishia kipigo sasa tunataka kwenda kumuwezesha mwanamke kiuchumi na asiwe tegemezi katika familia hivyo tunaimani kwa njia hii migogoro ndani ya familia itapungua," amesema Mmari.
0 Comments