Header Ads Widget

UVCCM KILIMANJARO WAMTAKA SPIKA NDUGAI KUJIUZULU NAFASI YAKE.




NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro umemtaka Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu kutokana na kwenda kinyume na Rais Samia Suluhu Hasani.


Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa UVCCM mkoa, Ivan Moshi alisema kuwa,  wamasikia na wengine kuona kioja kama si kiroja Job Ndugai (mb) na Spika wa bunge akipinga wazi jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya Chama cha Mapinduzi ambazo zimejikita katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kukopa fedha Tsh 1.3 Trilioni kutoka Benki ya Dunia 
 

Alisema kuwa, umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro katu haukufurahishwa na viroja vya Spika Ndugai kwa lengo lake la kumkatisha tamaa Rais na Mwenyekiti wa Chama kwenye jitihada zake za kuwaletea watanzania maendeleo. 


"Umoja wa vijana tukakumbuka hekima ya Shaban Robert katika andiko lake la kusadikika alipohimiza na kutia moyo wapenda maendeleo kwa kusema “KAMA WATU WANAOKUSUDIWA KUWA MWENGE KWA WENGINE WANGALIKUWA WAKINGOJEA SHANGWE LA WATU KABLA YA KUANZISHA MAKUSUDI YAO  MAENDELEO KATIKA MAISHA YANGALIADIMIKA”


 Alisema umoja wa vijana(UVCCM) Mkoa wa Kilimanjaro unamtia moyo Rais katika jitihada zake za kimaendeleo kwa kumuhimiza kukazana kutekeleza Ilani ya CCM ambayo inaakisi maendeleo ya watu pasina kungojea shangwe za ndugu Job Ndugai.


Mwenyekiti huyo alidai kuwa, Umoja wa vijana pamoja na kumuunga mkono kwa dhati Rais lakini unatoa Rai kwa Spika kujiuzulu nafasi yake ya Spika wa Bunge. 


"Msingi wa hoja hii ni undumilakuwili wa spika wetu ambaye hapo awali alipongeza mikopo hii na baadae kupinga vikali, inaonekana wazi tatizo sio mkopo bali ana lake" alisema Moshi.


Aliongeza kuwa, Chama cha Mapinduzi tangu TANU na ASP kimemea kwenye bustani ya ukweli  na kanuni za mwana TANU zilituasa kuwa wakweli kwa kusema NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO hivyo UVCCM mkoa wa Kilimanjaro umeamua kusema ukweli huu ambao unamtaka Spika Ndugai ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima yake na bunge. 


Alisema kuwa Waswahili wanasema “MSIBA WA KUJITAKIA HAUNA KILIO” hivyo fitina na unafiki wa Spika Ndugai unamuwajibisha mwenyewe. 


Moshi alisema kuwa, Umoja wa vijana mkoa wa Kilimanjaro unaamini msingi wa kanuni zake tuliyoirithi tokea TANU inayosema “NITAJIELIMISHA KWA KADRI YA UWEZO WANGU WOTE NA KUTUMIA ELIMU YANGU KWA FAIDA YA WOTE” 


Hata hivyo Mwl Nyerere katika andiko lake la TUJISAHIHISHE  amesema kujielimisha maana yake ni kutafuta ukweli wa mambo kwa msingi wa hoja hiyo spika wa bunge Ndugai amepuuza kanuni za chama kwa kushindwa kutafuta ukweli wa mambo hasa ujenzi wa madarasa yaliyojengwa nchi nzima kwa manufaa ya vijana wa kitanzania, na sio kwamba hajui bali fitina na uroho wenye choyo ya madaraka unamsakama.

Mwisho....

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI