Tume ya taifa ya umwagiliaji Mkoa wa Kilimanjaro imeanza kuchukua hatua kwa kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi sahihi ya maji kutokana na halo ya mabadiliko ya tabia ya nchi iliyopelekea maji kupungua katika baadhi ya skimu.
Mhandisi Said Ibrahim ni Meneja wa tume hiyo mkoa wa Kilimanjaro ambapo amesema hadi sasa hakuna athari za moja kwa moja ambazo zimeweza kujitokeza na kinachofanyika ni kujipanga ili zisitokee na kuleta madhara.
Amesema hatua nyingine ni pamoja na kuziba mifereji ili kuepusha upotevu Wa maji lakini pia kujenga mabwawa ambayo yatatumika katika kuhifadhi maji ambayo yatatumika pindi kutakapokuwepo na uhaba Wa maji.
0 Comments